#COVID19 Wizara ya Afya: Watanzania 800 wamefariki kutokana na COVID19 nchini

#COVID19 Wizara ya Afya: Watanzania 800 wamefariki kutokana na COVID19 nchini

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Naendelea kula bata Dodoma jamani.

Katika kongamano la kufanya tathimini na udhibiti linalofanyika mjini Dodoma, muwakilishi wa Wizara ya Afya amesema Watanzania 800 wamefariki kutokana na COVID19 hadi sasa.

Amesema Tanzania imepitia mawimbi manne ya COVID19. Ugonjwa bado upo lakini umeendelea kupungua kwa hali ya kuridhisha ambapo hadi wiki iliyopita kulikuwa na wagonjwa nane tu.

Hata hivyo, hatua za kujikinga ikiwemo kupata chanjo ili kupunguza maambukizi. Hadi sasa watanzania milioni 3.7 wamepata chanjo kamili. Hata hivyo inapaswa kuendelea kupata chanjo Zaidi ili kupata kinga Jamii.

Hadi sasa nchi imeidhinisha chanjo tano, ambazo watanzania wanaweza kupata chanjo yoyote kati ya hizo zilizopo. Na zinazidi kusogezwa mahali ambapo wananchi wapo mwanzo vilikuwa katika vitui 550 na kwa sasa vipo katika vituo vyote vya afya na huduma tembezi.
 
Tafadhali Sana msitaje majina ya 2021 maana itakua noma sana baadhi ya majina yatatikisa dunia.
 
Back
Top Bottom