Wizara ya Afya: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya COVID-19

Kuna Universal Health terms kwa magonjwa ya milipuko kutoka WHO, ukijifanya kwenda kinyume tu wanashughurika na wewe kwa namna yao.
Tulijifanya viburi, sasa tumebanwa kabisa lazima matamko yaongozane.
Ila ni jambo jema pia ukiona mambo hayaendi unakubali makosa...
 
Mwenzao huku anapambana na wanaochukua tahadhari.


 
Tamko “linawasihi na kuwasisitiza” watu wajichukilie hatua muhimu wao wenyewe.

Serikali inatamka wazi kwamba kila mtu abebe msalaba wake. Wao hawana mpango wa kuwabana wageni kuja wamepima wala kuongeza PPEs na Ventilators huko hospitalini..
 
Hamjali maisha ya watu kwa kuthamini msimamo wa mtu mmoja, mmeona viongozi wa juu wameanza kufa ndo mnajifanya kutoa tahadhari. Hakuna mwenye akili anayewaamini tena nyie walamba viatu wa Mfalme.

Watu mmesomeshwa kwa kodi za Watanzania lakini mnashindwa kuwaambia watanzania nini cha kufanya kwa wakati sahihi? Ni Sayansi gani mliyosoma iliyowahimiza kutokupima wagonjwa na kuwaacha wananchi wajitibu kwa kubashiri ugonjwa?

Dhambi hii haitawaacha salama Nyang'au nyie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…