#COVID19 Wizara ya Afya: Watu 2,117,387 sawa na 3.67% wamepata dozi kamili ya chanjo dhidi ya Corona

#COVID19 Wizara ya Afya: Watu 2,117,387 sawa na 3.67% wamepata dozi kamili ya chanjo dhidi ya Corona

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Kuanzia Januari 29 hadi Februari 6, 2022 visa vipya 252 vya COVID19 vilibainika kati ya watu 8,529 waliopimwa huku Dar es Salaam ikiongoza kwa kuwa na maambukizi 184.

Tangu Mlipuko kuripotiwa Machi 2020 hadi kufikia tarehe Februari 6, 2022 jumla ya watu 33,482 (7.6%) kati ya 442,566 waliopima walithibitika kuwa na maambukizi, 792 wamepoteza maisha.

Hadi Februari 6, 2022 dozi 9,845,774 za chanjo zilikuwa zimepokelewa Nchini, na jumla ya watu 2,117,387 (3.67%) wamepata dozi kamili tangu zoezi la utoaji chanjo kuanza.

88911D39-DE08-4DC1-9139-92B302004E35.jpeg


54899FFC-0671-4ED0-8954-03A075600930.jpeg
 
DSM pekee ina wakazi wa moja kwa moja wasiopungua 4m.

TZ ina watu takribani 60m. Tumenunua dozi 10m kwa 1.3t, sijui kama kuna riba!

Uingereza wamesema "Tu heli" na hiyo rona.

Dizaini kama vituo fulani vya habari wamevuta mpunga stahiki kuitangaza rona, ila muamko hamna, madhara hamna kitaa!

Ni bora watutangazie TOZO zetu zimeshafikia ngapi mpaka leo, maana walitangaza mara moja tu, JoNdu akabinafsishwa, na pia nasikia RISITI zinatakiwa tena, sijui falsafa ya kutotumia nguvu kazi kwenye kudai kodi imeishia wapi!
 
Back
Top Bottom