Joseverest
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 52,812
- 71,392
SIELEWI NISHIKE IPI NIACHE IPI
CONFUSED😵💫😵
CONFUSED😵💫😵
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dah! Ngoja nitasoma tena wiki ijayo maana leo nimeishia kwenye kichwa cha habari tu.JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UPOTOSHAJI WA MATAMKO YA VIONGOZI JUU YA MWENENDO WA UVIKO-19 NCHINI
Dodoma, Tarehe 20 Disemba, 2021.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imebaini taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii, kati ya taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu kwamba hakuna wimbi la nne la UVIKO-19 na ile iliyotolewa na Katibu Mkuu Afya kuhusu kuongezeka kwa maambukizi ya UVIKO-19.
Kimsingi taarifa zote hizi ni sahihi na wala hazipingani kabisa. Hii ni kwa kuwa, kuongezeka kwa maambukizi au Visa hakumaanishi kuwa tayari ni wimbi jipya la maambukizi na kitaalamu hii hujulikana kama resurgence of new cases (kuongezeka kwa maambukizi mapya). Kwa tafsiri halisi iliyotolewa na Stephen X. Zhang et al kwenye Jarida la Risk Management Health Policy la tarehe 13 Septemba 2021 “wimbi ni tofauti na ongezeko linalotokea ghafla na kwa kipindi kifupi (resurgence); ili kusema kuna wimbi jipya ni lazima hali ya ongezeko iendelee kwa kipindi fulani (walau kati ya siku 14-21)”.
Hivyo, kwa maelezo haya ya kitaalamu wananchi wapuuze upotoshaji wa taarifa sahihi za viongozi wote wawili na zimetolewa kwa wakati tofauti kama mwendelezo wa Serikali kuwasiliana na Umma. Aidha, wananchi wanakumbushwa kuendelea kuchukua tahadhari na kujikinga kwani ugonjwa wa UVIKO-19 bado upo na maambukizi yamekuwa yakiongezeka. Wizara inaendelea kufuatilia mwenendo wa ugonjwa huu na itakuwa inatoa taarifa kulingana na mabadiliko kadri yanavyotokea kwa mujibu wa takwimu za kila siku.
Imetolewa na;
Prof Abel N. Makubi
Katibu Mkuu (Afya)
View attachment 2051611
HahahahahaAnachapa kazi,mnataka aende wapi kariakoo?
Haa Wakati Wa MzilankendeAnachapa kazi,mnataka aende wapi kariakoo?
NakaziaUyo waziri mkuu hizo piko anazopakaa kichwani zimemuharibu ubongo, muongo muongo sana alafu hachagui pakuongopea yaani mpaka msikitini anaongea tu uongo
HaaIle ya kusemea msikitini ya kwamba chuma kina hali njema na kinachapa kazi na yenyewe walikanusha?
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu Au nasema uongo ndugu zanguNakazia
Ndiyo Ukweli WenyeweMsema kweli ni mpenzi wa Mungu Au nasema uongo ndugu zangu
Kimsingi taarifa zote hizi ni sahihi na wala hazipingani kabisa. Hii ni kwa kuwa, kuongezeka kwa maambukizi au Visa hakumaanishi kuwa tayari ni wimbi jipya la maambukizi na kitaalamu hii hujulikana kama resurgence of new cases (kuongezeka kwa maambukizi mapyaJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.