Wizara ya Afya nchini Kenya imetoa mwongozo mpya kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa wa Ebola, huku ikisisitiza umuhimu wa kutambua ishara za maambukizi mapema na kutafuta huduma za matibabu kabla hali haijawa mbaya.
Katika taarifa yake, wizara imeeleza kuwa dalili za awali za Ebola zinaweza kufanana na magonjwa mengine ya kawaida, jambo linaloweza kufanya baadhi ya watu kuchelewa kutafuta matibabu.
Kwa mujibu wa wizara, dalili hizo ni pamoja na homa, uchovu mkali, maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli, koo kuuma, kutapika na kuharisha.
Dalili zinaweza kujitokeza kati ya siku mbili na 21 baada ya mtu kuambukizwa virusi vya Ebola.
Wizara imewataka wananchi waliokuwa na uwezekano wa kuambukizwa na wanaoanza kuonyesha dalili hizo kutafuta msaada wa kitabibu mara moja, badala ya kujitibu nyumbani au kuendelea na shughuli zao za kawaida.
Soma pia Visa vya Ebola Kenya vyafikia 8, Muhudumu wa Hospitali ya Nairobi aambukizwa