Wizara ya Afya nchini Kenya imetoa taarifa kwa wananchi kuhusu namna virusi vya Ebola vinavyoenea, dalili za ugonjwa huo na hatua zinazoweza kuchukuliwa kuzuia maambukizi.
Hatua hiyo inakuja wakati Kenya ikiendelea kukabiliana na visa vya Ebola, huku serikali ikiimarisha ufuatiliaji wa wagonjwa na watu waliokuwa na mawasiliano ya karibu na walioambukizwa.
Kwa mujibu wa mwongozo wa afya, Ebola huenea kupitia kugusana moja kwa moja na damu au majimaji ya mwili wa mtu aliyeambukizwa, yakiwemo matapishi, mate, mkojo na kinyesi. Virusi hivyo vinaweza kuingia mwilini kupitia ngozi yenye michubuko, macho, pua au mdomo.
Maambukizi yanaweza pia kutokea mtu anapogusa vitu vilivyochafuliwa na majimaji ya mgonjwa, kama mashuka, nguo na vifaa vya matibabu.
Hata hivyo, Ebola haisambai kwa njia ya hewa kama mafua, na mtu aliyeambukizwa hawezi kueneza ugonjwa huo kabla ya kuanza kuonyesha dalili.
Dalili za Ebola ni pamoja na homa, uchovu, maumivu ya kichwa na misuli, kutapika na kuharisha. Dalili hizo zinaweza kuanza kati ya siku mbili na 21 baada ya mtu kuambukizwa.
Wizara inawahimiza wananchi kunawa mikono mara kwa mara, kuepuka kugusa majimaji ya mwili ya wagonjwa bila kinga na kutafuta ushauri wa wahudumu wa afya wanaposhuku wameambukizwa.
Watu waliokuwa karibu na mgonjwa wa Ebola wanashauriwa kuwajulisha wahudumu wa afya ili waweze kufuatiliwa na kupata msaada unaohitajika.
Wizara imesisitiza umuhimu wa kupata taarifa kutoka kwa vyanzo rasmi, badala ya kusambaza uvumi unaoweza kusababisha hofu isiyo ya lazima.
Soma pia