Unko T
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 200
- 266
Wa-Salaaam!
Katika hizi siku kadhaa nimeona matangazo ya Halmashauri mbali mbali zinatafuta vijana kufanya shughuli ya anwani za makazi na postikodi. Kwa kweli muitikio ulikua ni mkubwa sana, kwa macho yangu nimeshuhudia sio chini ya bahasha 5000 - 6000 kwa kazi wanayohitajika vijana 250 wenye umri wa miaka 18-35. Nikawa najiuliza hawa ni vijana walioliona au kusikia tangazo ndani ya siku mbili tatu, kwa maana Kuna wale ambao hawakuliona na wale wenye miaka 36 kuendelea na kuna wale wasiokua na elimu ya kidato cha nne kuendelea (ambao ndio wengi zaidi)
Serikali ya Rais Samia Suluhu kupitia Wizara mpya ya Ajira, je wana mikakati ipi ya ki-ubunifu kutatua tatizo la ajira, kwa hali iliyopo ni kubwa na ni bomu linalohesabu dakika.
Kuna kitu sikubaliani nacho, kwamba vijana wa kitanzania hawapendi kufanya kazi au wanasubiri Ajira na Serikali haina ajira za kuwapa. Huu ni mtazamo hasi unao onesha kuwa serikali inataka kukimbia jukumu muhimu la kuboresha maisha ya mtanzania. Vijana wanaweza na wana shauku kubwa ya kufanya kazi na wana elimu na ujuzi lakini kazi hakuna.
Kuna ule mpango wa mikopo ya halmashauri kwa vijana na wanawake. Ule mpango sio suluhu ya kujiajiri. Mikopo imejaa siasa na kujuana na wengine hupiga dili humo humo. Mikopo inahitaji watu wawepo kwenye vikundi, je vikundi ndio mustakabali wa kuanzisha start up companies? Mikopo hii imekaa kuzalisha mama lishe na machinga na sio wajasiriamali wenye ndoto kubwa za kutengeneza biashara za kuajiri mamilioni ya watanzania hapo baadae. Kama tuna taasisi ya kukopesha wanafunzi wa elimu ya juu, kwanini tusi unde taasisi ya kukopesha vijana wenye maono na malengo ya kuanzisha “biashara serious”?
Ni muda wizara ya ajira kutueleza mpango mkakati iliyonayo katika suala hili, kwa hali ilivyosasa ni kama wizara hii haipo kwa kuwa shughuli na mipango yake haionekani kulinganisha na wizara kama ya afya, utamaduni na michezo, nishati n.k.
Huu ni mtazamo na maoni yangu.
Shukrani.