Wizara ya Ajira ina mipango gani bunifu kutatua tatizo la ajira nchini?

Wizara ya Ajira ina mipango gani bunifu kutatua tatizo la ajira nchini?

Hata mimi nilishudia nikapatwa na mshangao tangazo yaani tangazo limetoka usiku asubuhi vijana kibao wanagombea fursa.
 
Mimi tatizo nalo liona kwenye ajira kuwa chache ni kwamba eneo la kufanya ajira ni dogo sana na sisi tumeridhika kuanzia wazee mpaka vijana na ikitokea serikali inaongeza eneo la kuzungusha uchumi tunasema huko hakutakiwi kupelekwa maendeleo wapaache hivyo hivyo Sasa hizo ajira zitatoka wapi? Jamani tuombe Kila mtu kijiji chake kipelekwe huduma zote muhimu mbona hizi ajira zitakosa watu? Maana zitapatikana za kuajiliwa na kujiajili kwa wingi, imagine vijiji vyote tulivyonavyo vikiwa na mazingira mazuri ya kufanya biashara na kutoa ajira hivi Kuna mtu atakosa ajira kweli? Kila kijiji kiwe na masoko, maduka, viwanda ikiambatana na umeme, maji, barabara, shule, hospitali vya serikali na binafsi, mahoteli, vyuo Kila kijiji kikiwa na vyuo vyake hata Veta tu Kila kijiji na nyumba za kisasa zinazohitaji vitu vya kisasa hapo ajira kwanini zikosekane? Mahakama Kila kijiji na viwanja vya ndege Kila kijiji acha mkoani peke yake Kila kijiji kiwe na stendi ya mabasi ya kisasa tayari hizo ni ajira, vituo vya mafuta Kila kijiji , majumba ya kufanyia biashara yaani hapo ndo tumekwama kiasi cha kugombania ajira za sehemu moja mijini peke yake hivyo kama tunapenda ajira kwa Kila mtu basi vijiji vigeuke sehemu za kuleta mzunguko wa pesa kama mjini.
 
Kuna miradi imelala miaka na miaka na ingeweza kupunguza changamoto ya ajira kwa vijana mfano mzuri ni mradi wa liganga na mchuchuma sijui kuna shida gani pale.
Mirada hiyo tangu miaka ya sitini jamani
 
Back
Top Bottom