Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Akitolea ufafanuzi kuhusu suala hilo leo, tarehe 26 Januari, 2026 jijini Dodoma, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, amesema wizara yake inaungana na Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha mgogoro unafanyiwa kazi na kukamilika.
''Hatua hiyo itahakikisha maeneo yanaendelezwa kwa kuzingatia mpango, na hivyo kuondoa migongano ya matumizi, kutunza mazingira, na kuweka nadhifu miji yetu''. Amesema
Pia soma ~ Mbunge Musukuma azichapa na ‘mwekezaji’
Kwa mujibu wa Dkt. Akwilapo, uendelezaji wowote unaofanyika sharti uzingatie sheria za uendelezaji miji, ikiwa ni pamoja na kupata vibali vyote vinavyotolewa na mamlaka zote za serikali. Kwa sasa, wataalamu wa Wizara wameungana na TAMISEMI kushughulikia suala hilo, na baada ya uchunguzi kukamilika, kutatolewa taarifa rasmi ya pamoja.
Uamuzi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuingilia kati sakata hilo unafuatia kusambaa kwa picha mjongeo katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ikionesha Kamati ya Fedha na Uchumi ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita ikilazimika kusimamisha shughuli za mradi wa ujenzi wa vibanda vya maduka kwenye eneo la viwanja vya CCM Katoro, huku ikidaiwa mwekezaji kuingia mipaka ya serikali ya kijiji katika Kitongoji cha Katoro Center kilichopo mji mdogo wa Katoro mkoani Geita.