DOKEZO Wizara ya elimu imeachia shule za binafsi msingi zifanye zitakavyo? Watoto wanasoma masaa 12 na hata zaidi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,311
Reaction score
15,640
Kwa muda mrefu, shule binafsi za msingi zimekuwa na utaratibu wa kupitiliza muda wa masomo kwa madarasa ya mitihani, kiasi cha kuwafanya watoto wakae darasani kwa saa nyingi kupita uwezo wa kawaida wa binadamu.

Cha kusikitisha, serikali haionekani kujali hali hii.

Ni jambo la kushangaza kuona kuwa elimu ya msingi imegeuzwa kuwa mzigo mzito kwa watoto, hadi kufikia hatua ya kuwafanya wakae darasani kuanzia saa 12 alfajiri hadi saa 1 jioni.

Je, wamiliki wa shule hizi wanatambua uwezo wa mtoto wa kuelewa na muda wake wa kukaa darasani? Inaonekana ubinafsi na ushindani wa ufaulu unawaumiza watoto, huku kukiwa hakuna wa kuwatetea.

Watoto wanakonda, afya zao zinatetereka, na mbaya zaidi, baadhi ya shule hulazimisha madarasa ya mitihani kubaki bweni bila ruhusa ya wazazi kuwaona. Wazazi wanapopata fursa ya kuwaona watoto wao, mara nyingi wanakutana na hali inayoumiza moyo.

Ni jambo la kushangaza kuona hata wanafunzi wa darasa la nne wakikumbwa na hali hii, huku darasa la saba likigeuka kuwa kipindi kigumu zaidi kuliko elimu yoyote, kuanzia msingi hadi chuo kikuu.

Mbali na muda mrefu wa masomo, hata mahitaji ya lishe kwa watoto hayazingatiwi. Katika umri huu wa ukuaji, wanapaswa kupata lishe bora, lakini badala yake, wanapewa chakula kilekile—ugali, wali, maharage, na makande—bila kuzingatia virutubisho wanavyohitaji.

Nani atawatetea watoto hawa dhidi ya tamaa za kibiashara za wamiliki wa shule? Ni jukumu la serikali, kupitia Wizara ya Elimu na TAMISEMI, kudhibiti hali hii kwa maslahi mapana ya watoto wetu. Ikiwezekana, mitihani ya shule za msingi ifutwe kabisa ili kukomesha mateso haya yanayosababishwa na tamaa ya biashara kwa kisingizio cha ufaulu.

Tunaiomba serikali ichukue hatua madhubuti na kutumia jopo la wataalamu si tu kudhibiti hali hii, bali pia kuwaelimisha wamiliki wa shule kuhusu mbinu bora za ufundishaji zinazozingatia ustawi wa watoto.

Soma pia KERO - Shule ya Bungo Mlimani ni changamoto, wanafunzi wanachelewa kutoka

 
Kwanini wazazi msilalamike kwenye uongozi wa shule hizo, au wasilisheni wizara ya elimu madhara wayapatayo watoto kusoma muda mrefu, nanyie wazazi kisha muiombe Wizara mnataka ifanye nini.

Kwasasa mtaambiwa kama hutaki muamishe mwanano mpeleke shule nyingine.
 
Ipo shule ya msingi huku ninapoishi wanafunzi wa darasa la saba wanatoka saa tatu usiku. Wamiliki hizi shule za private wana upumbavu wa kushangaza mno.
Inasikitisha aisee..kisa tu ufaulu wa juu kwa shule zao
 
Mkuu shule zote za private kwa sasa zinahuu utaratibu sababu zimeona wengine wanafanya na wanafaulisha zaidi yao. Hapo ni wizara kuingilia kati
 
English Medium School, (EMS, )
Oops
 
Maxence Melo naomba kwa nafasi yako usaidie kupaza sauti na ikiwezekana kuwepo hata midahalo itakayowaamsha wizara husika
 
Hivi huwa mnawapeleka watoto wenu huko EMS watoto wenu kwa ajili ya nini ?
 
Mkuu shule zote za private kwa sasa zinahuu utaratibu sababu zimeona wengine wanafanya na wanafaulisha zaidi yao. Hapo ni wizara kuingilia kati
Kama utaratibu ndio huo ili kupata matokeo mazuri, usitegemee serikali kukusaidia kwenye hilo. Nchi hii inaangalia matokeo.

Hapo ni wewe mzazi uchague, umlete huku kwetu au umbakishe huko private, na upambane na hali yako.

Andaa pesa mpeleke boarding, au mtoe umlete huku shule za kata, uondoe mashaka.
 
Yaani inaboa sana aisee yaani mtihani wa shule ya msingi unakua na tension kuliko mitihani ya vidato na university
 
Yote Tisa kumi Kuna shule ipo Mvuti ukishuka Mvuti unapanda bodaboda buku mpaka kwenye hiyo shule inaitwa M*l*n hiyo shule ni ya wasabato hapo kwenye hiyo shule ni siku Moja tu ndiyo unapumzika j'mosi Kuanzia wanafunzi na walimu.

Kuanzia j'pili vipindi vinaanza saa 10 alfajili mpaka saa 4 usiku kwenye hiyo shule hata kama wewe mwalimu umetafuta kazi miaka kumi ukipata kazi hapo ukimaliza miezi mitatu wewe ni mwanaume .

huyo mama mwenye hiyo shule anatesa walimu pamoja na wafanyakazi balaa Kwa kifupi ni mshenzi niliwahi kufanya kazi kabla sijajikita kwenye mitikasi mingine

Kiukweli hizo shule binafsi zinauhuni mwingi sana sahivi nimesikia yule mama anataka walimu kutoka mikoani ili hata wakifika wakinyanyasika iwe ngumu Kwa hao walimu kuacha kazi Kwa kuwa wanataka mbali ratiba yake ni ngumu mno na mshahara hauzidi laki 4.

Kuna walimu wanne wa madarasa Tofauti waliajiriwa January mwaka huu mwezi wa pili hawakutaka kuendelea walisepa sababu ratiba ngumu mno na manyanyaso hivyo wanafunzi wanateseka sana bila wazazi kujua.

Pia ili waweze kufanya mambo Yao ya hovyo ni kosa kubwa mno Kwa mwalimu kuwa na namba ya mzazi hawaruhusu ilo kutokea ili wazazi wasijue kinachoendelea ukigundulika mwalimu unamawasiliano na mzazi unafukuzwa kazi maana wanajua Siri zao mzazi atazijua mzazi wanawasiliana nae wenyewe.

Wanafunzi wanatakiwa waandike herufi Yani sky letters pamoja na ground letters Kwa kutumia rula ili zinyooke kama wewe ni mwalimu mpya haujajua hiyo mbinu mwandiko ukionekana haujanyooka ni balaa hawajatumia rula ni msala mkubwa hivyo inabidi ujiongeze uandae notes ndogo ubaoni ili wasichelewe kumaliza maana wanatumia rula.

Hiyo shule madereva wakipeleka wanafunzi shuleni asubuhi wakishafika wanabadilisha nguo zao wanavaa nguo za saidia fundi wanaanza kututusa mchanga pamoja na kufanya shughuli nyingine kama kuchimba mashimo kufyeka au kulima.

Yani hapo tulikuwa tunapaita ( sobibo) hiyo shule jaribuni kwenda kufanya kazi Kuanzia walimu na wanafunzi wote chamoto mtakiona ipo Mvuti ni balaa kila aliyefika alirusha Taulo uwanjani.

Nilijifunza kitu kabla hujampeleka mwanao shule za private fanya utafiti kama hiyo shule wazazi wangejua kama watoto wao wanateseka mno wasingewapeleka.

Hiyo shule wamejaa ndugu hapo kama hauna undugu nao Kaa pembeni maana wamejaa wamasai balaa wanamanyanyaso balaa.
 
Ni shule gani iyo mbona hakuna kitu kama icho
 
Yaani inaboa sana aisee yaani mtihani wa shule ya msingi unakua na tension kuliko mitihani ya vidato na university
Kwao biashara inapendeza watoto wakifaulu kwa wingi, hata ikiwa ni kwa kuwafundisha mtihani, wewe mzazi jiongeze.
 
Ipo shule ya msingi huku ninapoishi wanafunzi wa darasa la saba wanatoka saa tatu usiku. Wamiliki hizi shule za private wana upumbavu wa kushangaza mno.
Wanatafuta elimu kwa ugumu sana za wakati elimu sio vita. Elimu inatakiwa ipatikane ktk njia nyepesi na rafiki na pasipo na ushindani.
 
Mkuu shule zote za private kwa sasa zinahuu utaratibu sababu zimeona wengine wanafanya na wanafaulisha zaidi yao. Hapo ni wizara kuingilia kati
Ni ujinga kutumia nguvu na rasilimali nyingi zaidi kupata kitu cha kawaida. Naona hao ELIMU wanaitafsiri kwa ugumu sana. Elimu ni zaidi ya 'A' wanazozitaka
 
hata za serikali mkuu mtoto wangu mdogo wa std 4 anaingia class saa 12:30 kutoka saa 11 jioni huu ni ukatili wa hali ya juu wao wanachowaza na results tu , enz zetu sisi hayo madarasa ya chini ilikiua ni kutoka shule saa sita na tulikua vinenge mbaya,
 
Kunashida kubwa sana kwenye elimu ya sasahivi aisee. Na mamlaka wala hazichukui hatua yoyote kunusuru watoto. Darasa la 3 mtoto anapewa counterbooks 8 halafu zote Quire 4. Inasikitisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…