Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Imagine,tena kwa watoto aisee. Huu utaratibu kwa sekondari na kuendelea si tatizo. Ila primary school? Ni ujingaWanatafuta elimu kwa ugumu sana za wakati elimu sio vita. Elimu inatakiwa ipatikane ktk njia nyepesi na rafiki na pasipo na ushindani.
Leo nlikuwa nimeka nikaona mtoto wa jirani ametoka shule saa 12 jioni nikawa najiwazia watoto wanashinda shule muda wote, hawajifunzi mambo mengine ni shule mwanzo mwisho, shule sio mambo yote mtoto akifika form 2 inabidi angalau awe anajua kaz zingine na kuweza kuzifanya kwa ufasaha hizo zitakuwa plan B za baadayeKwa muda mrefu, shule binafsi za msingi zimekuwa na utaratibu wa kupitiliza muda wa masomo kwa madarasa ya mitihani, kiasi cha kuwafanya watoto wakae darasani kwa saa nyingi kupita uwezo wa kawaida wa binadamu.
Cha kusikitisha, serikali haionekani kujali hali hii.
Ni jambo la kushangaza kuona kuwa elimu ya msingi imegeuzwa kuwa mzigo mzito kwa watoto, hadi kufikia hatua ya kuwafanya wakae darasani kuanzia saa 12 alfajiri hadi saa 1 jioni.
Je, wamiliki wa shule hizi wanatambua uwezo wa mtoto wa kuelewa na muda wake wa kukaa darasani? Inaonekana ubinafsi na ushindani wa ufaulu unawaumiza watoto, huku kukiwa hakuna wa kuwatetea.
Watoto wanakonda, afya zao zinatetereka, na mbaya zaidi, baadhi ya shule hulazimisha madarasa ya mitihani kubaki bweni bila ruhusa ya wazazi kuwaona. Wazazi wanapopata fursa ya kuwaona watoto wao, mara nyingi wanakutana na hali inayoumiza moyo.
Ni jambo la kushangaza kuona hata wanafunzi wa darasa la nne wakikumbwa na hali hii, huku darasa la saba likigeuka kuwa kipindi kigumu zaidi kuliko elimu yoyote, kuanzia msingi hadi chuo kikuu.
Mbali na muda mrefu wa masomo, hata mahitaji ya lishe kwa watoto hayazingatiwi. Katika umri huu wa ukuaji, wanapaswa kupata lishe bora, lakini badala yake, wanapewa chakula kilekile—ugali, wali, maharage, na makande—bila kuzingatia virutubisho wanavyohitaji.
Nani atawatetea watoto hawa dhidi ya tamaa za kibiashara za wamiliki wa shule? Ni jukumu la serikali, kupitia Wizara ya Elimu na TAMISEMI, kudhibiti hali hii kwa maslahi mapana ya watoto wetu. Ikiwezekana, mitihani ya shule za msingi ifutwe kabisa ili kukomesha mateso haya yanayosababishwa na tamaa ya biashara kwa kisingizio cha ufaulu.
Tunaiomba serikali ichukue hatua madhubuti na kutumia jopo la wataalamu si tu kudhibiti hali hii, bali pia kuwaelimisha wamiliki wa shule kuhusu mbinu bora za ufundishaji zinazozingatia ustawi wa watoto.
View attachment 3258406
Aisee mbona kama jela. Yote tisa kumi ni hapo kwenye mateso kwa watoto aisee. Hii ipo hata kwenye shule za masista japo mi mkatoliki ila huo ni ukweli na siwezi mpeleka mtoto wangu kwenye hizo shule za masista maana kiukweli mtoto anaweza athirika kisaikopijia. Wazazi tunawajibu kufuatilia haya mambo kwenye hizi shule maana serikali kwenye hili haioni tatizo etiYote Tisa kumi Kuna shule ipo Mvuti ukishuka Mvuti unapanda bodaboda buku mpaka kwenye hiyo shule inaitwa M*l*n hiyo shule ni ya wasabato hapo kwenye hiyo shule ni siku Moja tu ndiyo unapumzika j'mosi Kuanzia wanafunzi na walimu.
Kuanzia j'pili vipindi vinaanza saa 10 alfajili mpaka saa 4 usiku kwenye hiyo shule hata kama wewe mwalimu umetafuta kazi miaka kumi ukipata kazi hapo ukimaliza miezi mitatu wewe ni mwanaume .
huyo mama mwenye hiyo shule anatesa walimu pamoja na wafanyakazi balaa Kwa kifupi ni mshenzi niliwahi kufanya kazi kabla sijajikita kwenye mitikasi mingine
Kiukweli hizo shule binafsi zinauhuni mwingi sana sahivi nimesikia yule mama anataka walimu kutoka mikoani ili hata wakifika wakinyanyasika iwe ngumu Kwa hao walimu kuacha kazi Kwa kuwa wanataka mbali ratiba yake ni ngumu mno na mshahara hauzidi laki 4.
Kuna walimu wanne wa madarasa Tofauti waliajiriwa January mwaka huu mwezi wa pili hawakutaka kuendelea walisepa sababu ratiba ngumu mno na manyanyaso hivyo wanafunzi wanateseka sana bila wazazi kujua.
Pia ili waweze kufanya mambo Yao ya hovyo ni kosa kubwa mno Kwa mwalimu kuwa na namba ya mzazi hawaruhusu ilo kutokea ili wazazi wasijue kinachoendelea ukigundulika mwalimu unamawasiliano na mzazi unafukuzwa kazi maana wanajua Siri zao mzazi atazijua mzazi wanawasiliana nae wenyewe.
Wanafunzi wanatakiwa waandike herufi Yani sky letters pamoja na ground letters Kwa kutumia rula ili zinyooke kama wewe ni mwalimu mpya haujajua hiyo mbinu mwandiko ukionekana haujanyooka ni balaa hawajatumia rula ni msala mkubwa hivyo inabidi ujiongeze uandae notes ndogo ubaoni ili wasichelewe kumaliza maana wanatumia rula.
Hiyo shule madereva wakipeleka wanafunzi shuleni asubuhi wakishafika wanabadilisha nguo zao wanavaa nguo za saidia fundi wanaanza kututusa mchanga pamoja na kufanya shughuli nyingine kama kuchimba mashimo kufyeka au kulima.
Yani hapo tulikuwa tunapaita ( sobibo) hiyo shule jaribuni kwenda kufanya kazi Kuanzia walimu na wanafunzi wote chamoto mtakiona ipo Mvuti ni balaa kila aliyefika alirusha Taulo uwanjani.
Nilijifunza kitu kabla hujampeleka mwanao shule za private fanya utafiti kama hiyo shule wazazi wangejua kama watoto wao wanateseka mno wasingewapeleka.
Hiyo shule wamejaa ndugu hapo kama hauna undugu nao Kaa pembeni maana wamejaa wamasai balaa wanamanyanyaso balaa.