DOKEZO Wizara ya elimu imeachia shule za binafsi msingi zifanye zitakavyo? Watoto wanasoma masaa 12 na hata zaidi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wanatafuta elimu kwa ugumu sana za wakati elimu sio vita. Elimu inatakiwa ipatikane ktk njia nyepesi na rafiki na pasipo na ushindani.
Imagine,tena kwa watoto aisee. Huu utaratibu kwa sekondari na kuendelea si tatizo. Ila primary school? Ni ujinga
 
Leo nlikuwa nimeka nikaona mtoto wa jirani ametoka shule saa 12 jioni nikawa najiwazia watoto wanashinda shule muda wote, hawajifunzi mambo mengine ni shule mwanzo mwisho, shule sio mambo yote mtoto akifika form 2 inabidi angalau awe anajua kaz zingine na kuweza kuzifanya kwa ufasaha hizo zitakuwa plan B za baadaye
 
Aisee mbona kama jela. Yote tisa kumi ni hapo kwenye mateso kwa watoto aisee. Hii ipo hata kwenye shule za masista japo mi mkatoliki ila huo ni ukweli na siwezi mpeleka mtoto wangu kwenye hizo shule za masista maana kiukweli mtoto anaweza athirika kisaikopijia. Wazazi tunawajibu kufuatilia haya mambo kwenye hizi shule maana serikali kwenye hili haioni tatizo eti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…