Wizara ya Elimu imeshindwa kuandaa audio na video ya vipindi vya masomo mbalimbali?

Wizara ya Elimu imeshindwa kuandaa audio na video ya vipindi vya masomo mbalimbali?

Ukiacha hiyo yake kama ataitaja, lakini kuna nyingine iitwayo www.shuledirect.co.tz
Pia ukiacha hiyo na yake kama ataitaja, kuna Open Discussion Forums: The Home of Critical Thinkers!

Ni very powerful and robust, with batteries included, inaweza kutumika kufundishia kuanzia kindergarten mpaka university and beyond, see

Open_D.png
Geog_maths.png
Maths_labels.png
Coding.png
Coding_x.png
AIntel.png
 
Mimi ninaendesha kipindi kila siku Online na wanafunzi wangu karibu wote wanashiri vzr sn. Yaani hapa hata wakitakiwa kurudi vyuoni, mtihani ukiwa wiki moja baada ya kufungua wanapasua vzr. Nipo chuo flani, vijana walitakiwa wafanye mtihani mwezi mei

Sent using Jamii Forums mobile app
Mhhh siku hizi Mianzini Shule ya Msingi kimekua Chuo?
 
Mimi ya serikali hayanishangazi, kinachonishangaza ni jinsi shule za private zimeshindwa kuwa na hizi videos na audios pamoja na rasilimali walizonazo.
 
Haya ni mawazo akiyekurupuka usingizini.

Hivi wewe unajua Tanzania hii kuna maeneo hakuna mtandao wa internet kabisa?
Karne hii ya kidigitali wizara hii inafanya ? Vifaa vipo, walimu wapo wa kurekodi, nini shida?

Kwa kila topiki tena na nyenzo za kufundishia

Hii Wizara iamke usingizini
 
Karne hii ya kidigitali wizara hii inafanya ? Vifaa vipo, walimu wapo wa kurekodi, nini shida?

Kwa kila topiki tena na nyenzo za kufundishia

Hii Wizara iamke usingizini
Kauli yako inaonesha hukai sana hapa tz au unaishi mjini na family yako mambo safiii! Kuna maelfu ya watu hawajawahi kununua redio
 
Karibuni sana Open Discussion Forums wakuu imhotep tindo Prishaz na wengine.

Kwa kifupi kuhusu hii platform:

Welcome to Open Discussion Forums -- The Home of Critical Thinkers!, a completely free knowledge & information exchange platform! Register or Log in, choose your favorite forum and start posting or replying to topics. Help others to learn by sharing with them what you have!

For more details, see Welcome To Open Discussion Forums

Open Discussion Forums is steadily gaining its due attention, in 2018, Open Discussion Forums was ranked number 32 in the 2018 list of Africa’s Movers and Shakers in Corporate Online Learning, see also Africa’s Movers and Shakers in Corporate Online Learning 2018
 
Haya mawazo ya masaki-dar Ila sio huku kwetu kupata tuu network ya kuongea shida je hiyo ya internet ndio balaaa nzito kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua unafiki wa mtu wa watu huwa haujifichi milele. Kuna wakati nia ya mtu katika jambo huonekana kwa urahisi.

Watanzania na viongozi wetu kwa ujumla si wapenda maendeleo. Hatuna nia ya dhati kulitoa taifa hapa lilipo. Kama wapo watu wenye uchungu basi ni wachache sana.....

Maana tazama, tokea uhuru changamoto za kimaendeleo bado ni zile zile za kimsingi, ujinga, maradhi na umasikini. Na hakuna jitihada za dhati kutokomeza hili. Watu wanapigana na umasikini kibinafsi na si kitaifa.

Sasa kama swala la corona linachukuliwa kimzaha sana huku ile hali mambo mengi yanasimama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi sijaelewa bado alichokusudia mleta uzi.
Namie ndio ilibidi niombe ufafanuzi mana nashangaa eti Wizara ya Elimu ndio ifundishe kupitia audio na video watoto wakiwa majumbani kipindi ichi. Basi na wakati wa kurudi mashuleni wapelekwe wizara ya elimu waendelee kusomeshwa tu, serikali itajenga mabanda wizarani ya madarasa. Maana hakuna umuhimu wa kuwepo shule kama hili ni kazi ya Wizara ya Elimu kusomesha wanafunzi majumbani.
 
Karne hii ya kidigitali wizara hii inafanya ? Vifaa vipo, walimu wapo wa kurekodi, nini shida?

Kwa kila topiki tena na nyenzo za kufundishia

Hii Wizara iamke usingizini
Waache watoto wapumzike na wasubr pasaka!
Ndio maana watoto wasiku hizi wanadumaa sana kimwili na kiakili!
Shuleni kusoma, likizo tuition! Sasa wapumzike wapi? Kwa Sasa ni mda wa likizo ya corona! Ni mda wa kunawa Mara kwa mara kujikinga na covid-19!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namie ndio ilibidi niombe ufafanuzi mana nashangaa eti Wizara ya Elimu ndio ifundishe kupitia audio na video watoto wakiwa majumbani kipindi ichi. Basi na wakati wa kurudi mashuleni wapelekwe wizara ya elimu waendelee kusomeshwa tu, serikali itajenga mabanda wizarani ya madarasa. Maana hakuna umuhimu wa kuwepo shule kama hili ni kazi ya Wizara ya Elimu kusomesha wanafunzi majumbani.
Wizara haimaanishi watu waliopo kwenye makao makuu ya wizara ya elimu pekee, wizara ya elimu ni kubwa kuliko hapo. Wizara inainclude taasisi nyingi ikiwemo vyuo vikuu vya serikali, VETA , taasisi ya elimu, NECTA n.k. Kabla ya kuhamishiwa TAMISEMI hata shule zote za serikali pia zilikuwa sehemu ya wizara ya elimu.

Kwa sasa hivi wizara bado inasimamia shule kwenye mambo mengi ikishirikiana na TAMISEMI ikiwemo mitaala na viwango na nadhani hapo ndipo mtoa mada anataka wizara kuplay part. Wanaweza kufanya kazi na walimu kuandaa media resources za kufundishia wanafunzi na kuanza na mahali kutumika mahali ambapo kuna miundimhinu ya msingi kama umeme na internet na kuendelea kuongeza network hadi kufikia shule zote.

Si lazima ifanyike yote kwa pamoja lakini inaweza kuchukua hata miaka kumi, ila la muhimu ni kuanza. Wakati itapofikia vijiji ambavyo kwa sasa hakuna internet/umeme tutakuwa tumeshaboredha media resources zenyewe, kutakuwa na walimu wenye uzoefu wanaoweza kufundisha na ku-share uzoefu na wezao na pia kutakuwa na wanafunzi wengu ambao walipata elimu bora kutokana na improvements za jinsi ya kufundisha.
 
Karne hii ya kidigitali wizara hii inafanya ? Vifaa vipo, walimu wapo wa kurekodi, nini shida?

Kwa kila topiki tena na nyenzo za kufundishia

Hii Wizara iamke usingizini
Nadhani walimu wanatakiwa kuamka na kulifanyia kazi hilo wazo
 
Back
Top Bottom