matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 9,514
- 23,523
1: Watoto wadogo kabisa wanakatisha usingizi na kuamka saa 11 asubuhi wamejipanga kusubiri school bus. Hapo kurudi ni saa 11 jioni utadhani mzazi katoka kwenye utafutaji. Hapa haijalishi hata kama ni chekechea au darasa la kwanza.
2: Kibaya zaidi ikifika muda wa mitihani ya kitaifa darasa la nne au la saba. Hapo ili shule ifanye vizuri watoto watateswa balaa. Wengine wanahamishiwa camp, wengine wanaanza kuingia darasani saa 11/12 asubuhi huku wanausingizi utadhani wanajiandaa na UE.
Nilikutana na mwalimu mmoja mkenya anasema tena ingekuwa ni amri yake ilitakiwa waanze kusoma saa kumi usiku ( la saba na la nne). Anadai ndio muda akili inachaji sana.
Hii kitu wadau imekaaje? Mimi naona kama ni mateso ya kibiashara zaidi sio elimu.
Wote tumekubaliana hakuna ajira watoto wanawahishwa wapi? Kwa nini wasikae shule muda mfupi tu ili muda mwingi akili ipate nafasi ya ubunifu na akili ikue kwa utulivu?
Ni hayo tu.
Je hakuna muongozo wa kitaifa au ni Romania goli tu.