Wizara ya Elimu mnaugonvi gani na walimu/wakufunzi?

Wizara ya Elimu mnaugonvi gani na walimu/wakufunzi?

omeka

New Member
Joined
Sep 13, 2013
Posts
4
Reaction score
1
Watendaji wizara ya Elimu wanaugomvi gani na walimu/wakufunzi waliopo chini ya katibu mkuu?
Mkufunzi anakaa miaka 6 hajapandishwa cheo/daraja na hapewi sababu yoyote zaidi ya kuwa tunashughulikia.

2011 walikuja na walaka mpya wa kiini macho kwa wakufunzi kwa wengi wa wakufunzi imekuwa ni majanga tu maana kama umekaa miaka 6/7 hujapanda unakuja kuambiwa muundo umekupeleka mbele daraja moja inakuwa haina maana, labda wangempatia kwanza madaraja yote aliyopunjwa ndo wampatie mkufunzi huyu daraja la ukufunzi.

Madai ndo sielewi kabisa umedai toka 2011 mpaka leo unaambiwa yanashughulikiwa, mara yalishapelekwa utumishi toka 2012 ela ikipatikana tu utaingiziwa, jamaani hii ni haki kweli?

Pia wakufunzi wote wapo mikoani yaani nje ya Dar es salaam, unakuja wizarani kufuatilia madai yako unazungushwa wiki nzima bila mafanikio wala majibu yenye matumaini.

Idara ya ualimu kuanzia Mkurugenzi wake Mr Issah mpaka wachini yake hawana msaada wowote kwa wakufunzi, Lugha chafu wanatumia kuwajibu wakufunzi, na ahadi za uongo. mfano toka Issah kaingia madarakani wakufunzi masomoni hawasaidiwi kwa lolote zaidi ya kuahidiwa uongo na kulazimishwa kujazwa mikataba ya kukandamiza tu.akipata ajira nyingine serikalini akiomba ahame na taarifa zake wamekuwa wanasumbua sana.

Upande wa utumishi wizara ya Elimu ni karaha na majanga kwa wakufunzi, kuna jamaa anaitwa Minja anahusika na kupanda madaraja, anaweza akakaa na tatizo la mtu miaka 2 hajashughulikia, na jibu lake kila siku ni kuwa nashughulikia.
Madaraja ni miaka 4 kwa wanaoanza na 3 kwa wengine, cha ajabu mtu anakalishwa miaka 5/6/7 hajapanda bila maelezo ya maana, na unapopandishwa hawaangalii kama kama ulidhulumiwa nyuma mwisho unajikuta uliyekuwepo kazini miaka 10 na mwenya miaka 3 ni sawa ingawa unaelimu yakutosha kupandishwa na uzoefu na huna matatizo yoyote ya nidhamu.

Hivi hawa watendaji wanamatatizo gani, alafu wanatulea BRN na hizi stress wanazotupatia wanategemea nini?

Wakufunzi na walimu tuliobakishwa kwa katibu mkuu ni wachache sana hatufiki hata elf 5 lakini wanashindwa kutuhudumia kwa wakati. mfano sasa hivi walitakiwa mpaka waliopanda daraja mara ya mwisho 2010 wawe wameshapanda lakini mpaka wa 2008 wengi tu bado wanazungushwa, 2010 ndo wanajibiwa nyie bado sana, mpaka lini haijulikani tunaumizana jamani. na kuvunjana moyo wa kufanya kazi.

Wizara ijue wakufunzi wengi wamekata tamaa ya kufanya kazi, wako busy kutafuta mbinu nyingine ili familia zao ziwe na hali nzuri,na watoto wao waende shule nzuri,na wakijikita zaidi kwenye hizo mbinu zingine wanaoumia ni wanafunzi na jamii, walimu wanozalishwa katika hali ya stress za mwajiri ndo kama wa mwaka uliopita, mtaendelea kuja na BRN,1,2,3,4,5,6,..............................................................................................................................sisi tutaendelea kula hiyo mishahara yetu yenye mapunjo mengi,tukijikita zaidi kwenye mbinu zingine mpaka wizara itakapo jirekebisha na kututendea haki walimu/wakufunzi tuliopo kwa katibu mkuu.
 
Sisi ambao tunasubiri ajira si ndo balaaa had leo hatujaajiliwa
 
Sisi ambao tunasubiri ajira si ndo balaaa had leo hatujaajiliwa

Hakika ningelikuwa na uwezo ningemfukuza minja maramoja kwani amekuwa ni kero sana. Kwa kifupi anamatatizo mengi mosi nizembe nilishawah peleka barua akasema nitashughulikia akaweka ktk drop nilirud baafa ya miezi minne akaniuliza wee nan kwann hukuleta taarifa mapema nikamwambia nilikuja na nilikuachia barua ukaiweka ktk droo akasema wee kijana ni mwongo akaangalia akaiona barua ikiwa haijafanyiwa kaz nilisilitika saana.
 
Poleni wakufunzi\walimu wetu,nchi hii wanajijali sana wao kuliko watendaji wa chini ambao ndo wapokea lawama tu.
 
Shamba la bibi, huyo jamaa anashindwa kuelewa nn, anaona mtumishi akipanda daraja na mshahara kupanda atanufaika na inaonesha hata yeye anaishi maisha ya hali ya chini na watu kama hao ndiyo hawatakiwi kuongoza watu na kwan sirikali haioni matatizo ya watumishi imuondoe huyu kilaza?
 
protocol ni kwamba taifa jinga la kesho walimu wajiajiri afu watu waendele na system kama kawaida afu ideas without actions is vapour
 
Back
Top Bottom