Wizara ya Elimu Okoeni Kizazi

Wizara ya Elimu Okoeni Kizazi

Makupa

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
6,822
Reaction score
4,034
Tunapongeza sana maboresho yanayofanyika kwenye Elimu yetu haswa wakati huu wa serikali ya awamu ya Sita.

Mheshimiwa Rais tunaomba umwagize Waziri wa Elimu ahakikishe kuwa wanafumzi wa shule za msingi na haswa binafsi wanapata elimu inayoendana na hadhi na umri wa wanafunzi husika.

Tunayo mifano ya shule za binafsi ambazo wanafunzi wa darasa la saba wanaanza masomo kuanzia saa kumi na mbili asubui hadi saa tatu usiku kwa siku saba za wiki.
 
Tunapongeza sana maboresho yanayofanyika kwenye Elimu yetu haswa wakati huu wa serikali ya awamu ya Sita.Mheshimiwa Rais tunaomba umwagize Waziri wa Elimu ahakikishe kuwa wanafumzi wa shule za msingi na haswa binafsi wanapata elimu inayoendana na hadhi na umri wa wanafunzi husika.Tunayo mifano ya shule za binafsi ambazo wanafunzi wa darasa la saba wanaanza masomo kuanzia saa kumi na mbili asubui hadi saa tatu usiku kwa siku saba za wiki.
Sio saa kumi na mbili, Kuna shule moja sitaitaja iko mkoa x, dogo alisema mara nyingine wanaamshwa saa kumi na nusu na saa kumi na moja na nusu wawe darasani
 
Kwanini watoto wa sasa hivi wanasoma masaa mengi zaidi darasani, huku maarifa yakiwa madogo zaidi kulinganisha na vizazi viwili nyuma yao?

Kuna tatizo kubwa sana kwenye mfumo wetu wa malezi watoto wanakosa lishe bora na michezo, watoto wetu akili zao nzito sana.
 
Kwanini watoto wa sasa hivi qanasoma masaa mengi zaidi darasani, huku maarifa yakiwa madogo zaidi kulinganisha na vizazi viwili nyuma yao?

Kuna tatizo kubwa sana kwenye mfumo wetu wa malezi watoto wanakosa lishe bora na michezo, watoto wetu akili zao nzito sana.
Vidonge vya majira vinachangia sana watoto kuwa na hali hiyo
 
Jamani me naomba kuuliza nipo na mdogo wangu kafanya mtihani 2022 kapata ( D ) ya English, ( D ) ya Geography na ( D ) ya kiswahili Sasa kitu gan anaweza kusoma.
 
Akivuta bangi usishangae, saa 8 atamkuta nani nyumbani
Wapo wamejaa tele..muda huo washatoa mikeka nje wanaangalia wanaopita barabarani..au wako sebuleni wanaangalia Azam Tv zile tamthilia.
 
Kwanini watoto wa sasa hivi wanasoma masaa mengi zaidi darasani, huku maarifa yakiwa madogo zaidi kulinganisha na vizazi viwili nyuma yao?

Kuna tatizo kubwa sana kwenye mfumo wetu wa malezi watoto wanakosa lishe bora na michezo, watoto wetu akili zao nzito sana.
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo !
 
Back
Top Bottom