Chendembe
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 444
- 488
Nawasalimu kwa kutoa maoni yangu katika upangaji wa ratiba katika vyuo mbalimbali hapa nchini.
Naomba Wizara ya Elimu na wahusika kupitia ratiba za masomo vyuoni. Imekuwa kawaida sasa kuona ratiba hizo kupangwa kutokana na nafasi za walimu wa masomo vyuoni kuelekea vipindi vingine kuanzia usiku.
Kwangu naona vipindi vya usiku vinahatarisha maisha ya watoto wetu hususani katika majiji yetu. Pia, inashawishi vijana wengi kujihusisha na tabia chafu.
Kwa hali ya kuongezeka kwa udahili vyuoni na upungufu wa mabweni kwa sasa, ni hatari kwa maisha kwa wanaosoma vipindi hivyo ukizingatia baadhi ya maeneo ambayo wanachuo wengi upanga vyumba.
Nashauri ratiba iendane na muda wa kazi wa Serikali na sio nafasi ya mwalimu.
Nawasilisha