Wizara ya Elimu wafuteni machozi watoto hawa

Milonji

Senior Member
Joined
May 26, 2022
Posts
166
Reaction score
510
Nani atasikiliza sauti zao, watoto hawa wanaolia.

Nani atawafuta machozi yao yanayo sombwa na Maji.

Nani atayaona machozi yao ikiwa watabaki kulia ndani kwa ndani.

Chaliko ninawasilisha kilio chao na kupaza sauti zao ili Mamlaka zinazohusika zisikie Changamoto wanazopitia Wanafunzi hawa.

Tangu kufunguliwa kwa Shule Wanafunzi wa Shule hii wamekuwa wakisoma kwa kusuasua Sana.

Kuna wakati wanakaa siku zaidi ya tatu bila kusoma na Kuna masomo hawajasoma kwa muda mrefu.

Hawa Wanafunzi wa kidato Cha Nne na cha Pili watafanyaje MITIHANI yao ya Taifa kama hawakufundishwa.

Nina waonea Huruma Wanafunzi hawa ambao hawafundishwi kisa Mwenye Shule ameshindwa kuwalipa walimu Mishahara na Walimu wameweka mgomo wa Chini kwa Chini.

Ninawaonea Huruma kwa sababu wamelipa Ada ambayo Wazazi wameitafuta kwa Hali na Mali kwa ajili ya kuwapatia watoto maarifa amabayo hawapewi.

Ninawaonea huruma kwa sababu Elimu ni haki yao na hakuna anaye wajali.

Ninawaonea huruma kwa sababu hawa ni Ndugu zetu.

Wizara ya Elimu tusaidiane kulishughulikia hili haraka iwezekanavyo ili watoto wapate haki yao ya Msingi.

NCHI: TANZANIA
MKOA: DODOMA
WILAYA:. DODOMA CC
KATA:. NKUHUNGU
SHULE:. NKUHUNGU SEKONDARI

Ndugu zangu, Sikilizeni Sauti, Yaoneni na kuyafuta Machozi ya Wanafunzi wa NKUHUNGU SEKONDARI ili ndoto zao zipate Kutimia.

Taarifa kwa;

Wadau wa Elimu

Afisa Elimu Kata ya Nkuhungu.

Afisa Elimu Jiji la Dodoma.

Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma.

Wizara ya Elimu.

TAMISEMI

Wenu Milonji.
 
Malalamiko kama haya muwe mnapeleka sehemu husika
 
Malalamiko kama haya muwe mnapeleka sehemu husika
Asante Mkuu Slowly kwa ushauri. Japo napenda kukuhakikishia kuwa JAMII FORUM ni platform ambayo imesaidia Watu wengi Sana.

Kuna wakati nilikomaa na Watu wa TANESCO hapa Jukwaani. Mwisho wa siku waliwalipa Watu fidia zao japo nje ya Muda.
 
Hiyo shule ni ya serikali au binafsi??
 
Ya binafsi Mkuu.
Kama ni ya binafsi na Wazazi wamelipa ada zao,Basi wapeleke malalamiko yao police, maana Kama umelipia huduma alafu hiyo huduma yenyewe hupati,basi huo tayari ni wizi wa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu!!
 
Kama ni ya binafsi na Wazazi wamelipa ada zao,Basi wapeleke malalamiko yao police, maana Kama umelipia huduma alafu hiyo huduma yenyewe hupati,basi huo tayari ni wizi wa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu!!
Umemalizaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…