Wizara ya elimu yaagiza shule zote za Dar Es Salaam kufungwa kwa siku 2 kupisha kongamano la nishati

Wizara ya elimu yaagiza shule zote za Dar Es Salaam kufungwa kwa siku 2 kupisha kongamano la nishati

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema kufuatia taarifa ya Serikali kuhusu agizo la baadhi ya Watumishi wa Umma kufanyia kazi nyumbani, Wizara hiyo inaelekeza Shule zote za Msingi, Sekondari na Vyuo katika Mkoa wa Dar es Salaam kufungwa kwa siku mbili January 27 na January 28, 2025.

Taarifa iliyotolewa leo January 26,2025 na Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa imesema “Tangazo hili ni kwa Vyuo na Shule za Serikali na Binafsi, Wadau wote wa elimu wanaombwa kuzingatia tangazo hili ili kuepusha changamoto za usafiri zinazoweza kujitokeza kutokana na kufungwa kwa baadhi ya barabara, masomo yataendelea kama kawaida kuanzia January 29, 2025”

Hatua hii inakuja ili kuepusha usumbufu utakaosababishwa na kufungwa kwa barabara kutokana na ugeni mkubwa wa Watu wanaokuja kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Kuhusu Nishati utakaofanyika Jijini Dar es salaam kesho na keshokutwa.

Mkutano huo unaandaliwa kwa pamoja baina ya Serikali ya Tanzania, Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika ambapo Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Marais wa Nchi za Afrika 24, Wawakilishi wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Afrika 21, Wakuu wa Taasisi za Kimataifa sita wakiwemo Rais wa Benki ya Dunia, Rais wa Benki ya Afrika na Rais wa Taasisi ya Rockefeller na Washirika wa Maendeleo watano watashiriki Mkutano huo na pia jumla ya Washiriki wengine 2,600 wa ndani na nje ya Tanzania wamejisajili kwa ajili ya Mkutano huo.
#MillardAyoUPDATES
Tanzania kila kitu ni shida tu.
 
Kuna shule ziko Kawe, Chanika, Msongora Kigamboni nk. Hali itakwaje. Na je wale walio boarding?
 
Tushaambiwa atakuwepo Rais wa Taasisi ya Rockefeller sasa hapo bado mnashangaa kitu gani?
Acha kazi sizimame,wenye kazi zao wapo mjini..tukae kwa kutulia.
 
Back
Top Bottom