Wizara ya Elimu yaomba kutumia Tsh. 1,968,212,534,000.00 katika mwaka 2024/25

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia chini ya Waziri Mhe. Prof. Adolf Mkenda imeomba bunge kupitisha Makadirio ya Bajeti ya Wizara yenye jumla ya Shilingi 1,968,212,534,000.00.

VIPAUMBELE

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania laidhinisha zaidi ya shilingi Trilioni 1.97 zilizoombwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele vitano vya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 ili kuleta mageuzi ya Elimu nchini.

1. Kuendelea na utekelezaji wa sera na mitaala, mapitio ya sheria na kuandaa miongozo ya utoaji elimu na mafunzo nchini.

2. Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (amali na amali sanifu).

3. Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya msingi, sekondari na ualimu.

4. Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya juu na kuendeleza tafiti, matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu.

5. Kuendelea na utekelezaji wa Sera na Mitaala, Mapitio ya Sheria na kuandaa Miongozo ya Utoaji Elimu na Mafunzo Nchini.

Wizara ya Elimu imesema kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 wataweka mkazo kwenye Elimu ya Ujuzi (Skillis Oriented) ili kuwawezesha wahitimu wa ngazi mbalimbali za Elimu kujiajiri na kuajiri wengine.
1715076768829.png

1715076808867.png

1715076721596.png
 
Attachments

Zitumike ipasavyo wasijinufaishe wao tu
 
Hi hela nyingi sana na mbona mishahara ya walimu bado midogo hivo? 1.9 trillion ni nyingi sana, almost 18% ya budget ya nchi? Madawati bado ni shida, madarasa bado ni shida, nyenzo za kufundishia bado ni za kizamani na hapo bado mtaala wetu ni wa kizamani.
 
Hii ni trillioni?

Mishahara + Bodi ya Mikopo + Kuwalisha boarding School + Maendeleo ya Shule
 
Kwa wale wavivu kusoma
Hapo ni trillioni Moja na billion mia Tisa sitini na nane na milioni mia mbili kumi na mbili na laki Tano na elfu thelathini na nne
 
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia chini ya Waziri Mhe. Prof. Adolf Mkenda imeomba bunge kupitisha Makadirio ya Bajeti ya Wizara yenye jumla ya Shilingi 1,968,212,534,000.00.

VIPAUMBELE

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania laidhinisha zaidi ya shilingi Trilioni 1.97 zilizoombwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele vitano vya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 ili kuleta mageuzi ya Elimu nchini.

1. Kuendelea na utekelezaji wa sera na mitaala, mapitio ya sheria na kuandaa miongozo ya utoaji elimu na mafunzo nchini.

2. Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (amali na amali sanifu).

3. Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya msingi, sekondari na ualimu.

4. Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya juu na kuendeleza tafiti, matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu.

5. Kuendelea na utekelezaji wa Sera na Mitaala, Mapitio ya Sheria na kuandaa Miongozo ya Utoaji Elimu na Mafunzo Nchini.

Wizara ya Elimu imesema kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 wataweka mkazo kwenye Elimu ya Ujuzi (Skillis Oriented) ili kuwawezesha wahitimu wa ngazi mbalimbali za Elimu kujiajiri na kuajiri wengine.
View attachment 2983308
View attachment 2983310
View attachment 2983305
 
Back
Top Bottom