Wizara ya Fedha yatoa mafunzo ya ugavi kwa waandishi

Wizara ya Fedha yatoa mafunzo ya ugavi kwa waandishi

KIJICHO PEVU

Member
Joined
May 4, 2024
Posts
69
Reaction score
49
Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Sera za Usimamizi wa Ununuzi wa Umma, imeendesha mafunzo maalum kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii kuhusu mnyororo wa ugavi, ikiwa ni juhudi za kuimarisha uelewa na ushirikiano kati ya vyombo vya habari na serikali katika kusimamia rasilimali za umma.

Mafunzo hayo yalifanyika jijini Morogoro na yalifunguliwa rasmi na Kamishna wa Idara ya Sera za Usimamizi wa Ununuzi wa Umma, Dkt. Frederick Mwakibinga. Akizungumza wakati wa ufunguzi, Dkt. Mwakibinga alieleza kuwa vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika kuhakikisha uwazi, uwajibikaji, na ufanisi katika mfumo wa ununuzi wa umma.

“Waandishi wa habari ni daraja kati ya serikali na wananchi. Ili waweze kutekeleza wajibu huo ipasavyo, ni muhimu kuwajengea uwezo wa kuelewa mifumo ya ununuzi wa umma, hasa kuhusu mnyororo wa ugavi,” alisema Dkt. Mwakibinga.

Mtoa mada katika mafunzo hayo alikuwa ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dkt. Maige Mwasimba, ambaye alielezea kwa kina dhana ya mnyororo wa ugavi, changamoto zilizopo, na nafasi ya vyombo vya habari katika kusaidia kuboresha mifumo ya usimamizi wa manunuzi ya serikali.

Dkt. Mwasimba aliwataka waandishi kuandika kwa kina na kwa uelewa sahihi kuhusu michakato ya ununuzi wa umma, ili kuibua changamoto na kusaidia mabadiliko chanya katika mfumo wa ugavi.

Mafunzo haya ni sehemu ya mkakati wa wizara hiyo kuimarisha uwazi na uelewa kwa wadau mbalimbali kuhusu mnyororo wa ugavi, hasa ikizingatiwa kuwa eneo hilo lina mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa.

Waandishi walioshiriki waliipongeza wizara kwa kuandaa mafunzo hayo, wakieleza kuwa yamewapa mwanga mpya kuhusu masuala ya ununuzi wa umma na jinsi wanavyoweza kuchangia katika kuhakikisha matumizi bora ya fedha za umma kupitia taarifa wanazotoa kwa umma.


 
Ukisikia wizara na idara za serikali zinamalizia bajeti kwa nguvu ndio kama hivi seminar za ajabu ajabu ili mradi tu fedha zitumike kabla mwaka wa fedha haujaisha
 
Ukisikia wizara na idara za serikali zinamalizia bajeti kwa nguvu ndio kama hivi seminar za ajabu ajabu ili mradi tu fedha zitumike kabla mwaka wa fedha haujaisha
Wailete seminar hiyo na huku JF nasi tuambulie makombo.
 
Back
Top Bottom