Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Hii nchi kila kitu ni drama; waziri wa katiba na sheria na watumishi wa ofisi yake tayari wameandaa kinachoitwa kampeni ya elimu ya katiba mpya na bajeti yake inalengwa kwa mwaka wa kwanza kutumia si chini ya bilioni tisa.
Watumishi wote wa ofisi yake wameshajiwekea ratiba hakuzunguka nchi nzima kwa miaka miwili kama siyo mitatu. Malipo waliyojiwekea ni kila mtumishi kulipwa 220,000 kila siku kwa kipindi chote cha kampeni
Makundi mbalimbali wataitwa kujustfy elimu hiyo vikiwemo vyama vya siasa na taasisi za kiraia.
Swali langu ; haya mambo yanajadiliwaga wapi na kupitishwa? Hii mikakati ya kutumia fedha za umma kipindi hiki ambacho kuna mdororo wa kiuchumi inawekwa na nani? Kwanini hatuoni kwamba wapo watanzania wasiopata japo mlo mmoja kwa siku?
Hizi kampeni wamexipa miaka mitatu kwa kuanzia katiba gani kampeni inafanyika miaka mitatu? Wanaotoa elimu ni wanasheria na watumishi wa umma ambao hata katiba iliyopo hawana uelewa nayo......
Tunakwenda wapi watanzania? Kwanini tusirudi mezani kujadiliana haya mambo na kuja na uelewa wa pamoja badala ya watumishi wa umma kujimegea fedha za umma ; let assume viongozi wote wa wizara na watumishi wanajilipa kwenda kwenye kampeni kazi ofisini anafanya nani?