KIKWAZO CHA KATIBA MPYA YENYE MFUMO WA VYAMA VINGI NI CCM!
Katiba iliyopo ni ya mfumo wa chama kimoja ambacho ni CCM na ilitungwa na CCM mwaka 1977.
Tanzania hatuna mfumo wa vyama vingi, bali tuna mfumo wa chama kimoja (CCM), ambamo kuna vyama vingi ndani yake. Kwa ufupi tuna vyama vingi ndani ya mfumo wa chama kimoja - CCM!
Kamwe CCM hakiwezi kuleta katiba mpya yenye mfumo wa vyama vingi maana itakuwa ni kujimaliza chenyewe.
Katiba mpya ni mpaka CCM itoke madarakani kama Kenya walivyoiondoa kwanza KANU ndiposa ikaja katiba mpya. Kwanza tuondoe kikwazo ambacho ni CCM, ndiposa tutapata katiba mpya.
La sivyo tutaendelea na maigizo (seasons) ya katiba mpya bila kupata katiba mpya.
Tulikuwa na season ya "kamati" ya katiba mpya, ikaja "tume" ya mabadiliko ya katiba, mara kikaja "kikosi" kazi, na sasa umekuja Mkakati wa Taifa wa Elimu ya Katiba kwa Umma (MTEKU) hadi 2026.
Pasina kukiondoa CCM madarakani, seasons zitaendelea bila ya kupata katiba mpya. Tunapigwa danadana za freestyle football mpaka tunaona kizunguzungu!
Credit:
Gwappo Mwakatobe