Wizara ya katiba na sheria imejizindulia utaratibu wa kula pesa za walipa kodi kwa kampeni ya elimu ya katiba mpya 2024/2026; waanza kuandaa mikutano

Kibaraka
Nimeona hata clouds tv kwenye clouds 260 asbh hii wameshaanza hicho wanachokiita elimu kuhusu katiba kule Zanzibar. Hii nchi aliyetulaani sijui ni nani! Time ya Warioba walizunguka njia nzima kukusanya maoni ya wananchi. Na Kwa majibu Yale ya wananchi iliashiria kabisa katiba mpya inahitajika na wanaielewa katiba iliyopo na ndio maana walitoa maoni Yao. Zilitumika pesa nyingi kwa kazi Ile,Sasa wananchi tunashangaa Kwa hiki kinachoendelea. Utumislaji mbovu wa Kodi za wananchi na nia ovu ya kuchelewesha katiba mpya kupatikana. Wananchi tusikubali kabisa huu ujinga.
 
Nchi ngumu hii. Watu wapo kula kwa urefu wa kamba walizojikadiria wenyewe. Uzuri walishaambiwa wale.
 
Kibaraka
Kwanza ni mawazo ya kipumbavu sn kutoea elimu kwa miaka 3, kwanini isiwe kwa miezi 2? kikosi kazi kilifanya kazi gani miezi 6 yote?
Wanatuona sisi wananchi ni wajinga hatuna akili. Hii ni dharau kubwa ni ipo siku yatafikia mwisho haya
 
Unapata kihoro ukiwa wapi ewe mlala hoi? Huna taarifa Rais alituruhusu tule kwa urefu wa kamba zetu?
Ili uumie zaidi, per diem ni 1m, pesa ya mafuta ya gari tutavuta 20m, bado pesa ya matengenezo ya gari 20m. Hii mipesa yote hii ni kwa siku 20 tu. Na kwa mwaka huu wa pesa, tutaenda kula nchi mara 20. Piga hesabu wewe mwenyewe ujue nitavuta kiasi gani.

Nasema hiviii: Mwaka huu nisipojenga gorofa kila mkoa, niite nguchiro.
 
KIKWAZO CHA KATIBA MPYA YENYE MFUMO WA VYAMA VINGI NI CCM!

Katiba iliyopo ni ya mfumo wa chama kimoja ambacho ni CCM na ilitungwa na CCM mwaka 1977.

Tanzania hatuna mfumo wa vyama vingi, bali tuna mfumo wa chama kimoja (CCM), ambamo kuna vyama vingi ndani yake. Kwa ufupi tuna vyama vingi ndani ya mfumo wa chama kimoja - CCM!

Kamwe CCM hakiwezi kuleta katiba mpya yenye mfumo wa vyama vingi maana itakuwa ni kujimaliza chenyewe.

Katiba mpya ni mpaka CCM itoke madarakani kama Kenya walivyoiondoa kwanza KANU ndiposa ikaja katiba mpya. Kwanza tuondoe kikwazo ambacho ni CCM, ndiposa tutapata katiba mpya.

La sivyo tutaendelea na maigizo (seasons) ya katiba mpya bila kupata katiba mpya.

Tulikuwa na season ya "kamati" ya katiba mpya, ikaja "tume" ya mabadiliko ya katiba, mara kikaja "kikosi" kazi, na sasa umekuja Mkakati wa Taifa wa Elimu ya Katiba kwa Umma (MTEKU) hadi 2026.

Pasina kukiondoa CCM madarakani, seasons zitaendelea bila ya kupata katiba mpya. Tunapigwa danadana za freestyle football mpaka tunaona kizunguzungu!

Credit: Gwappo Mwakatobe
 
Hizo ni mbinu tu za kuchelewa mchakato mzima wa kupata katiba mpya kwa maslahi ya kundi fulani linalohodhi madaraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…