Wizara ya Katiba na Sheria imetoa elimu ya utawala bora na masuala ya kisheria kwa viongozi wa serikali za mitaa na kamati za usalama, ili kuwawezesha kutoa huduma bora na za haki kwa wananchi, ikilenga kupunguza malalamiko ya wananchi na kuboresha ufanisi wa serikali katika utendaji kazi wake.