Wizara ya Kilimo yashirikiana na JKT kumaliza tatizo la mbegu kwa wakulima

Wizara ya Kilimo yashirikiana na JKT kumaliza tatizo la mbegu kwa wakulima

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amezungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Machi 24, 2022:

“Tutashirikiana na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika uzalishaji wa mbegu za mazao mbalimbali, ili kuhakikisha nchi inajitosheleza kwa uzalishaji wa mbegu bora.

“Lengo letu ni kumaliza tatizo la upatikanaji wa mbegu bora. Kwasasa mbegu huzalishwa na TARI kupitia Vituo 17 vya utafiti vya Wizara, na mashamba 13 ya Wakala (ASA), haya hayatoshi. Hivyo, Tunafanya ushirikiano huu kama jitihada ya kuziba upungufu wa mbegu za mazao muhimu.

“Tunafanya ushirikiano huu kama jitihada ya kuziba upungufu wa mbegu za mazao muhimu.”



Chanzo: Wizara ya Kilimo
 
Good move sahivi ukikamatwa unazurura maeneo ya jeshi ni mwendo wa kupalilia vitalu.
Tena wangeanza na wapiga debe wote ukikutwa tu unabebwa kambini ukapande miche
 
Hili halifiki popote na halitatatua chochote. JKT wanajua nini kuhusu uzalishaji wa mbegu?
 
Hivi ile sehemu wanafanya utafiti wa Mbegu Hapo ilonga, kilosa wanafanya nini

Ova
 
Back
Top Bottom