DOKEZO Wizara ya Madini ipige marufuku wachimbaji wadogo kutumia zebaki ili kutunza mazingira na kuuimarisha Afya za wananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Hellow Tanganyika!

Uharibifu wa mazingira ni mkubwa Kanda ya Ziwa, Nia ni njema kuruhusu wachimbaji WADOGO, ila usimamizi wa karibu ni muhimu.

Serikali chini ya wizara ya madini itengeneze centers za kuchakata udongo na mawe yenye dhahabu mchimbaji mdogo alipie gharama.

Huu uholela wa wachimbaji WADOGO kuharibu vyazo vya maji Kwa kutiririsha zebaki kwenye vyanzo vya maji ni chanzo kikuu Cha magonjwa ya saratani yanayoongezeka Kwa Kasi Kanda ya Ziwa.

Najua Kuna bunge linaendelea, lichukueni hili, na hata msipolichukua, IPO siku litafanyiwa KAZI.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
 
Wasipigwe Marufuku, hao ndio wanaolipwa Kodi Kwa wingi na kuchangia pato la Taifa na la kwao .

Pesa wanayoipata inazunguka humuhumu Tanzania , tofauti na mabeberu wanalinda mazingira lkn Pesa yote inaenda Nje .


Jambo la Msingi, Waelimishwe juu ya matumizi sahihi ya Zebaki kwao wenyewe ,Kwa wananchi wanaowazunguka na namna ya kulinda mazingira.



Hoja yako ni sawa na BASHE kusema Mwashamba ya Miwa, yageuzwe kua ya mpunga, Sukari tuagize nje .
 
Hakuna Mahali nimesema wachimbaji WADOGO wazuiwe hapana,

Kuchimba wachimbe, ila viroba vyao wapeleke kwenye centers zitakazoanzishwa chini ya wizara Ili kuchakata udongo na mawe kuwa dhahabu Kwa umakini, ubora wa juu zaidi.

Kumuelimisha mchimbaji mdogo ambaye hata choo tu kujenga hazingatii awapo kazini, awezeje kununua vitu vya gharama kubwa kuzuia maji ya zebaki yasiingie udongoni au kuingia kwenye vyanzo vya maji,

Hili linagitaji usimamizi wa wizara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…