1. Itungwe Sheria, Wenza wanapotengana, mwenye uwezo wa Kumtunza Mtoto kihuduma, ndîo apewe Mtoto.
Mwingine awe na Haki tuu ya kumwona Kwa utaratibu utakaowekwa.
Kwa sababu kûna weñye tàbia ya kung'ang'ania Watoto huku uwezo wa kuwatunza Hawana. Hii inapelekea Watoto wengi kukosa Haki ya Malezi Bora na wengi Ndoto zào huishia Njiani.
2. Mtoto asikae Kwa ndugu kama Wazazi wake wawili wàpo.
Ima akae Kwa Babaake au Kwa Mamaake.
3. Mtoto anahaki ya kumjua mzazi wake halisi.
Masuala ya kusema kitanda hakizai haramu humnyima Mtoto Haki ya kujua Wazazi wake halisi na hiyo kumharibia Maisha take yote na kizazi chake.
Hivyo sheria ya Kupima DNA ísiwe na mlolongo ili kuwapa Haki Watoto na wenye Mtoto.
Hii Sheria NI kama kweli Haki inahitajika, lakini kama NI geresha siô lazima.
4. Mtoto awe na Haki ya kuchagua Ûkoo íwe wa Mama au wa Babaake. Ikiwa kutatokea utengano.
Masuala ya kulazimisha ûkoo unatoka Kwa Baba au Mwanaume ni Haki endapo kuna Ndoa au Mtoto kalelewa na Baba au Mwanaume. Lakini Mtoto aliyelelewa Kwa upande wa Mama awe na Haki ya kuchagua majina na kuwa ûkoo wa ujombani, kiukeni.
5. Adhabu za Mtoto zilenge dhamiri ya Mtoto.
Mtoto àmbaye hajakusudia kufanya Kosa asiadhibiwe na Yule aliyedhamiria kufanya Makosa apewe adhabu inayolingana na Kosa lake.
6. Mtoto akiwa Yatima tangu kuzaliwa, au chini ya Miaka mitano. Apewe Haki ya Kurithi kwèñye familia atakayolelewa. Na atakayemlea apewe Haki ya kumfanya huyo Mtoto kuwa Mtoto wake Kwa njia ya adaptation hata kama ni ndugu yake.
Ikiwa Mtoto NI Yatima Kwa Mzazi mmoja, na Mzazi aliyebaki Hai akamtelekeza Mtoto huyo Kwa namna Moja ama ñyiñgine. Na kusababisha Mtoto huyo kulelewa na Kukuzwa na familia ñyiñgine isiyo ya ukoo wa huyo Mzazi aliyehai. Mtoto huyo atakuwa chini ya ukoo wa alikolelewa, ingawaje Sheria haitakataza mtoto kuambiwa ukweli kuhusu mzazi wake halisi.
Mzazi hatakuwa na Mamlaka ya kumchukya Mtoto huyo isipokuwa Kwa makubaliano na hiyari ya Mlezi WA huyo Mtoto.
Sheria hiyo itafaa zaidi kama Mtoto atalelewa Kwa zaidi ya Miaka Kumi,
7. Mtoto akishakuwa Mkubwa hatakuwa na wajibu wa Kumtunza Mzazi àmbaye hakumlea akiwa Mtoto.
Isipokuwa Kwa hiyari ya mtoto mwenyewe .
Mzazi àmbaye hakumlea Mtoto hatakuwa na Haki ya kumsumbua Mtoto wake na kumfanya Mtoto ataabike kwaajili yake isipokuwa atasubiri hiyari ya mtoto mwenyewe.
Hiyo ndîo HAKI.
8. Mtoto endapo atakufa atakuwa na haki ya kuzikwa upande aliolelewa Ikiwa hakutoa maelekezo Mengine.
Mtu yeyote ikiwemo Mzazi ambaye hakuhusika na Malezi ya mtoto aliyekufa hatakuwa na Haki ya kudai Mwili WA Mtoto na kwenda kuuzika atakako. Isipokuwa Kwa hiyari ya waliomlea Mtoto huyo.
9. Mtoto akikua na kufikisha Umri wa kuoa au kuolewa weñye mamlaka ya kuratibu shughuli nzima ya Ndoa íwe upande alipokuzwa na kulelewa.
Au Kwa hiyari ya waliomlea wanaweza kufanya vinginevyo
10. Mtoto akishakua atakuwa na haki ya kuchagua mwenza wake wa Maisha atakayemridhia pasipo kuingiliwa.
11. Ikitokea Mwanamke kudanganya na kumbambikia Mumewe Mtoto ambaye siô wake. Mtoto ataendelea kuwa Mtoto wa huyo Mwanaume wa kambo kisheria mpaka atakapofikisha Umri wa kujitegemea. Ikiwa Mtoto akataka kwenda Kwa Babaake halisi, huyo Baba halisi itampasa atoe fidia ya Pesa Kulingana na Maisha ya kipindi husika