Adhabu za viboko ni kudhalilisha na kuutweza utu wa mtoto nashangaa ulimwengu wa leo bado kuna watu wanaamini kwenye vipigo kama njia ya kutatua kosa.
...
Siungi mkono kufuta viboko, bali naunga mkono kupunguza viboko mashuleni
Kinachotokea sasa hivi tuna kopy taratibu za ulimwengu wa kwanza ambao wapo mbele yetu pengine kwa miaka 60 na kuendelea, unaweza kujiuliza wao walizuia hizo fimbo lini?
Nina mifano michache hapa; Marekani walizuia 1977, Ufaransa walizuia 2014, Australia walizuia 1985, Uingereza walizuia 1986 - unaweza kuona kabisa ni majuzi tu)
Wanao piga kelele sana kufuta viboko ni wale wazazi ambao watoto wao wanatumia mabasi ya njano ambao pengine ni 15% ya watoto wote wanaosoma ILA kwa sababu wao ndio wenye access na social media kelele zinaonekana ni nyingi. Ila ni ukweli pia hao watoto wa mabasi ya njano hata tukifuta vikobo wao hawata adhirika au hawata adhirika sana
Vijijini bado kabisa, huwezi kufuta fimbo; watoto watoro shule, wanapigana mitaani, wanaiba miwa, maembe, korosho, machungwa, mwingine leo sijui wa darasa gani kavunja kioo cha basi kwa jiwe nk nk nk unawezaje kuwarekebisha bila fimbo? hata Biblia imetuambia kuwa, tusiwanyime watoto fimbo
Kwa mtazamo wangu tukiingia huo mkenge wa kufuta fimbo; miaka 30 ijayo tutajutia na hatutaweza tena kurudi nyuma
Ifike mahala tutumie akili zetu kufikiri vitu vinavyo endana na mazingira yetu; Utafikiri wasomi wetu wanakwenda vyuoni kusomea kukopy na kupaste...kila kitu ukiuliza Msomi anakujibu wenzetu (ulaya) wanafanya hivi.... badala ya kujibu, mimi naona hivi........