Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 157
- 155
Serikali kupitia wizara ya Maji imehaidi kutuma timu ya wataalam na mitambo ya kisasakufanya utafiti maalum wa upatikanaji wa maji baridi katika maeneo yenye changamoto ya maji chumvi hususani katika wilaya ya Maswa na Meatu mkoani Simiyu.
Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Raslimali za Maji, Wizara ya Maji,Dkt George Lugomela(pichani) wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ipililo wilaya ya Maswa mara baada ya kukagua mradi wa maji katika kijiji hicho.
Amesema kuwa serikali inatambua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama inazozikabili baadhi ya vijiji na vitongoji vya wilaya hizo kwa kuwa maji yaliyopo katika maeneo hayo, kuwa na kiwango kikubwa cha chumvi .
“Kupitia wataalamu wetu, tutafanya utafiti wa kina ili kubaini vyanzo vya maji baridi vilivyoko chini ya ardhi. Tutatumia teknolojia ya kisasa kuhakikisha tunapata maji salama na yenye ubora kwa matumizi ya binadamu,”amesema
“Kupitia wataalamu wetu, tutafanya utafiti wa kina kubaini vyanzo vya maji baridi vilivyofichika chini ya ardhi. Tutatumia teknolojia ya kisasa kuhakikisha tunapata maji bora kwa matumizi ya binadamu,” alisema Dkt. Lugomela.
Aliongeza kuwa mitambo itakayotumika katika utafiti huo pia itajumuisha vifaa vya kuchunguza hali ya miamba chini ya ardhi, visima vya majaribio,na teknolojia za kuchuja chumvi endapo itahitajika.
Dkt Lugomela amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anafikiwa na huduma ya maji safi na salama ifikapo mwaka 2030, sambamba na malengo ya maendeleo endelevu.
“Hii ni hatua muhimu kuelekea kutimiza dhamira ya serikali ya kuhakikisha huduma za kijamii,hususan maji zinaimarika na kuwafikia wananchi wote mjini na vijijini,”amesema.