Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Tanzania sijui ni nani amewaloga watumishi wa umma. Kila wakikaa ofisini wanatafuta namna ya kuwafanya watu wasiende kuzalisha badala yake wakapange foleni kubishana na watumishi husika.
Tanzania watu wanaopanga kujikwamua kiuchumi lazima wanaripoti ofisi zifautazo kwa lengo la kuendesha biashara zao
1. Brella
2. Rita
3. TRA
4. TIC
5. TFDA na sasa imevunjwa nakuunda mamlaka mbili
6. WOSHA
7. FIRE
8. TCRA
Hawa wote wanatumia mifumo ya TEHAMA, tunaweza kusema wanajitambua.
9. Hawa Wizara ya mambo ya ndani. Wao wanatumia mifumo manual na kuzunguka kufolenisha watu.
Mhe. Rais amekuwa akizungumza kila wakati kuhusu matumizi ya TEHAMa; hawa wanaomsikiliza akiwemo huyu msajili wa taasisi za kiraia wa wizara ya mambo ya ndani hana ofisi popote isipokuwa Dodoma. Kwa kuwa hana ofisi anachofanya hataki kutengeneza mifumo watu wajaze online badala yake anataka azunguke nchi nzima alipwe fedha za umma kujidai anasajili makanisa, sijui whatsapp group nk. Huu siyo wizi wa rasilimali za taifa?
1. Huyu mtu ana tija kwa Taifa
2. Anapata wapi nguvu yakupingana adharani na azma ya Mhe. Rais yakutaka taasisi ziachane na manual system ziende kwenye TEHAMA
3. Fedha anazolipwa za kuzunguka mikoani hazitoshi kuunda mifumo watu wakaingia online wanakamilisha taratibu?
4. Mhe. Rais anajua kwamba movement za viongozi wa dini na wamiliki wa taasisi za kiraia kwenda Dodoma zimekuwa nyingi na ukifika hapo wizara ya mambo ya ndani hadi upate huduma lazima upoteze siku mbili au tatu? Watumishi wanatafuta majalada kwa tochi.
5. Je, Mhe. Rais anajua ni kiasi gani hawa watu wametumia kuhakiki taasisi jambo ambalo wangeweza kulifanya kwenye mfumo? Wanadai wanahakiki taasisi lakini hakuna siku wanafika kwenye taasisi wanakaa ofisini watu wanawafuata.
Tunao viongozi wanatumia vibaya madaraka yao badala ya kumsikiliza Mhe. Rais wanajisikiliza wenyewe.
Nashukuru Mhe. Rais ameelekeza Naibu Waziri akashughulikie mifumo, naamini ataanza na hawa wanaosumbua wananchi kwa kuwapangisha foleni. Lakini naamini pia serikali inaweza ikaona umuhimu wa kutumia mifumo kama ya RITA na BRELLA kufanya usajili badala ya kuingia gharama kuwapa tenda watu wengine wakati mifumo ipo na yote ni mali ya serikali.