Wizara ya Mambo ya Nje ni kiungo muhimu katika mafanikio ya serikali - Waziri Kombo

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema kuwa Wizara kupitia Balozi zake duniani imekuwa kiungo muhimu cha kufanikisha na kuchochea mafanikio ya Serikali katika sekta zote nchini, iwe kilimo, uchukuzi, biashara au nishati.

Waziri Kombo amesema hayo wakati wa kikao kati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) na Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Najma Murtaza Giga Katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma Agosti 11, 2026.

“Kwa ufupi balozi zetu zinahusika na kila chembe ya mafanikio yanayoonekana hapa nchini ikiwemo upatikanaji wa fedha za ujenzi wa miundombinu kama vile reli ya kisasa, ununuzi wa ndege, upatikanaji wa vibali vya safari za ATCL, makusanyo ya maduhuli kupitia utalii na mauzo ya visa kwa wageni na upatikanaji wa fursa za uchumi wa buluu”, alisema Waziri Kombo

Balozi Kombo aliendelea kueleza kuwa Wizara kupitia Balozi zake imetekeleza majukumu yake ya msingi kwa kuzingatia Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001, Toleo la Mwaka 2024 na kufanikiwa kupata mafanikio makubwa kwa manufaa ya nchi.

Mafanikio hayo ni pamoja na kupanua wigo wa uwakilishi, kuongezeka kwa fursa za biashara na uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje, kuimarika kwa uhusiano wa uwili, upatikanaji wa misaada na mikopo yenye masharti nafuu pamoja na kukua kwa matumizi ya lugha ya Kiswahili duniani.

Kwa upande wao, wajumbe wa Kamati wameipongeza Wizara kwa kazi nzuri inayofanya katika kuimarisha diplomasia na kulinda maslahi ya Tanzania na kuitaka kuongeza juhudi ili diplomasia ya Tanzania iendelee kung’ara duniani.

 

Attachments

  • IMG-20260811-WA0044.jpg
    148.2 KB · Views: 11
  • IMG-20260811-WA0045.jpg
    134.6 KB · Views: 10
  • IMG-20260811-WA0036.jpg
    90.2 KB · Views: 9
  • IMG-20260811-WA0037.jpg
    100.7 KB · Views: 11
  • IMG-20260811-WA0038.jpg
    105.4 KB · Views: 13

TOKA MAKTABA


Hatimaye wabunge wa bunge haramu la chama kimoja mjini Dodoma wajadili maazimio yaliyopo ktk waraka wa wabunge wa Senate na Congress kumpa Donald Trump rungu aweze kuwashughulikia Samia pamoja na wateuliwa wake

26 May 2026
Dodoma, Tanzania

Mwanzo -Mwisho Wabunge wa chama dola kongwe CCM Wachachamaa bungeni kutokana na Marekani Kutaka Kuwawekea Vikwazo Viongozi wa Serikali Tanzania


View: https://m.youtube.com/watch?v=Lqzt1cnif5oWabunge hawa wa CCM wameyaongea haya leo Mei 26, 2026, wakati wakichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje. Michango hii inakuja baada ya muswada kuwasilishwa katika kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Seneti la Marekani wenye lengo la kuwawekea vikwazo viongozi wa Tanzania kufuatia mauaji ya Oktoba 29 2025
 
11 Agosti 2026
Kwa upande wao, wajumbe wa Kamati NUU (ulinzi na Usalama) wameipongeza Wizara kwa kazi nzuri inayofanya katika kuimarisha diplomasia na kulinda maslahi ya Tanzania na kuitaka kuongeza

TOKA MAKTABA :
March 2026
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA (NUU) YATEMBELEA UJENZI WA GEREZA JIPYA, MAHAKAMA MTANDAO (VIDEO)

View: https://m.youtube.com/watch?v=_Kz-l9_dZ8E juhudi ili diplomasia ya Tanzania iendelee kung’ara duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…