Wizara ya Mawasiliano yaomba kuidhinishiwa Shilingi Bilioni 291.5 kwa mwaka wa Fedha 2025/2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 unaendelea leo, Mei 16, 2025, jijini Dodoma, ambapo hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa mwaka wa fedha 2025/2026 inawasilishwa na kujadiliwa.
"Sekta ya Mawasiliano na TEHAMA imekua kwa 7.6% mwaka 2023, ikichangia 1.4% kwenye pato la Taifa – takwimu hizi ni ndogo ukilinganisha na uhalisia. Kwa mwaka 2025/26 tunaanzisha Akaunti Maalum ya Uchumi wa Kidijitali (DESA) ili kupima kwa usahihi mchango wa sekta hii."

"Laini za simu zilizosajiliwa zimeongezeka kutoka milioni 73.5 Aprili 2024 hadi milioni 90.4 Aprili 2025" sawa na ongezeko la 22.9%, amesema Waziri wa Mawasiliano. Aidha, "watumiaji wa intaneti wamefikia milioni 49.3 kutoka milioni 37.3," sawa na ongezeko la 32.3%."

"Huduma za kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu nazo zimepanda kwa asilimia 23.9, huku idadi ya watoa huduma za miundombinu ikifikia 38, ikilinganishwa na 27 mwaka uliopita."

"Mwenendo huu unaonesha mafanikio katika kufikisha huduma za kidijitali kwa wananchi,"

Gharama za Mawasiliano na Data zazidi Kupungua

"Wastani wa bei ya dakika ndani ya mtandao bila kifurushi umeendelea kubaki Shilingi 26, na nje ya mtandao Shilingi 28 kati ya Juni 2024 hadi Aprili 2025, amesema Waziri."

"Gharama za data ndani ya kifurushi zimeshuka kidogo kutoka Shilingi 2.16 hadi 2.12 kwa MB. Vilevile, usajili wa vikoa vya intaneti umeongezeka kwa asilimia 11.3, kutoka 30,090 hadi 33,494 Aprili 2025."

Vipaumbele vya Bajeti ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa mwaka 2025/26

"Wizara Kujenga Miundombinu, Kuimarisha Usalama Mtandao na Kukuza Ubunifu 2025/26"

Wizara ya Mawasiliano na TEHAMA itajikita katika "kutunga sera mpya za TEHAMA, Anga za Juu na Startups, pamoja na marekebisho ya Sera ya Posta ya 2003."

Aidha, itakamilisha ujenzi wa "minara 758 kwenye kata 713" na kuendeleza ujenzi wa minara 636 vijijini.

Pia, Serikali itaunganisha "wilaya 11 na Mkongo wa Taifa" na wateja 90,000 na huduma za "Faiba Mlangoni Kwako".

Katika kukuza ulinzi wa mtandao, Wizara itaboresha uwezo wa Jeshi la Polisi kanda ya Mbeya na Mwanza, na kuwezesha mfumo wa kitaifa wa ufuatiliaji wa makosa ya mtandao.

Vilevile, Serikali itasimamia uanzishwaji wa vyuo viwili vya TEHAMA, vituo vinne vya bunifu kwa ngazi ya wilaya, na vituo vinane vya ubunifu katika mikoa mbalimbali.

MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YAMAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI KWA MWAKA WA FEDHA2025/26

Waziri wa Mawasiliano na TEHAMA amesema, "Katika mwaka wa fedha 2025/26, Wizara inakadiria kukusanya Shilingi bilioni 100.4 kutoka huduma za Mkongo wa Taifa."

Wizara inaomba kuidhinishiwa Shilingi bilioni 291.5 kwa matumizi, ambapo "Shilingi bilioni 14.4 ni matumizi ya kawaida, ikijumuisha mishahara bilioni 6.9 na OC bilioni 7.5."

Aidha, miradi ya maendeleo imepangiwa Shilingi bilioni 277, ambapo bilioni 98.4 ni fedha za ndani na bilioni 178.5 ni fedha za nje.
 

Attachments

Sema kikao cha fisiem.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Bajeti ya wizard ya ulinzi imepita?
Je bajeti ya wizard ya mambo ya ndani imepita?
Je wizard ya elimu bajeti imepita?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…