Wizara ya michezo acheni kumkuza Samatta peke yake, mnawakatisha tamaa 'maprofesheno' wengine

Victor wa happy

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2013
Posts
11,660
Reaction score
11,654
Hili jambo Linanikera sana mimi binafsi

Samatta amekuwa ndio kipenzi cha Serikali kwa wachezaji wanaopiga gozi nje ya nchi, anazungumzwa bungeni, anazungumzwa yeye peke yake ni Kama wanatengeneza picha kuwa ni yeye peke yake anayecheza huko ugaibuni wanasahau kuwa kwasasa wachezaji angalau wanaocheza nje ya nchi ni wengi tu sasa kumpongeza peke yake haifai

Najua kuwa samata anajitahidi kwa kiasi chake huko alipo lakini kuwekeza kwake peke yake sio picha nzuri

Jana nimemuona waziri mweye dhamana ya michezo akimpokea samata je ataenda kuwapokea na wengine?

Na waandishi wa habari walivyo sio watu wakujiongeza kila siku ubeligiji etiquette kwenda kumpongeza

Hili taifa letu nilaajabu ajabu hivi hadi nashindwa kuelewa

Kama mnatoa mailage kwa wachezaji wapeni heshima wote sio kuruka kuruka

Pale burundi kuna mchezaji anacheza uingereza ila huwezi kuona kelele Kama zinavyopigwa huku kwetu

Pale Kenya, Victor Wanyama anacheza uefa champions final lakini sioni wakenya wakipiga kelele km sisi

Uganda wanawachezaji huko ubeligiji lkn hawana kelele

Yaani sisi watanzania ni wakudeal na mambo madogo madogo tu

Mara wengine wanataka eti samata ajengewe sanamu maajabu haya!! Kwa lipi alilolifanya?

Serikali acheni kuendesha mambo kwa ushabiki wa mitandaoni.
 
Sion mantiki ya uzi wako.Samatta yuko na juhudi zaidi ya hao wengine.Anastahili pongezi.Nao hao wengine wakaze buti wafikie alipo tutawapongeza pia.
#motivation
 
Samatta ndio mchezaji pekee mtanzania kucheza ligi ya juu katika bara la ulaya....

Kachukua tuzo ya mchezaji bora mweusi ubelgiji

Kaisadia timu yake kubeba ubingwa wa ligi

Kaongoza kwa ufungaji katika kikosi chake cha genk

Kwanini asipongezwe?

Naamini hata wanyama akibeba UCL kenya watampongeza sana....

Acha majungu
 
Waziri anaacha usingizi wake kwenda kumpokea Samata akishuka kwa Turqish airline usiku wa manane. Wanyama akibeba CL hope tutamwona Uhuru akienda kumpokea airport.
 
Lakini Kaka wa Wanyama , Mac Mariga alibeba UCL akiwa na Inter Milani sidhani km walimtukuza hivi

Lkn yote kwa yote Samata anastahili sifa
 
Waziri anaacha usingizi wake kwenda kumpokea Samata akishuka kwa Turqish airline usiku wa manane. Wanyama akibeba CL hope tutamwona Uhuru akienda kumpokea airport.

wanyama kabla ya tottenham alikuwa scotland.. katwaa sana mataji ya kigi ya kule ila wakenya hawana shobo.. na ligi ya scotland ni kubwa kuliko ya ubelgiji..

kaka yake mac donald mariga alitwaa champions league na inter milan ila wakenya hawana shobo..

dada yake wanyama amecheza basketball women basketball usa ila wakenya hawana shobo..
 
ungetoa na mifano ya hao wengine hata wawili tu wanaofanya vyema na team zao na hawatukuzwi kama sammata, uzi ungekuwa umeutendea haki.

Anayofanya sammata anastahili heshima, kwani itawapa na wengine hamasa walau wafike hata ligi kuu za sweden, denmark turkey n.k.
 
samatta anastahili pongezi kwa yote aliyofanya.
 
Kama hao wakenya hawawasifii watu wao, hilo ni tatizo lao.
Sisi tunampaisha Samagoal mwanzo mwisho. Aliye juu msupport tu, usimngoje chini. Hao wachezaji wetu wengine nao wajitume kuvamia nyavu mpaka waimbwe kama Samatta anavyoimbwa Genk.
 
Mambo ya Mwakyembe saa nyingine hayaeleweki sijui anapiga bange yule
 
Kujengewa sanamu itakuwa ni ajabu la Dunia!
Hilo halitatokea, Samatta kwanza ni Muislam na anahofu ya Mungu pili ni Mndengereko hata picha wandengereko hawazipendi ndio maana hutoona sana picha za mababu na mabibi wa kindengereko
 
Nafikiri soka ya Tanzania tff wanaiua kabisa . Hawajafanya utafiti kujua ni wachezaji wangapi waliozaliwa Tanzania wapo nje wakicheza soka la kulipwa na wenye asili ya Tanzania. angalia ratiba ya ligi ilivyokuwa mbovu hata timu ya taifa imekosa muda wa kutosha kujiandaa na mazoezi na mechi za majaribio. Nafikiri kipindi cha tff ya tenga kingepata raisi wa Tanzania wa sasa mh Dr.Jpm soka la Tanzania lingekua juu sana.
 
Waziri anaacha usingizi wake kwenda kumpokea Samata akishuka kwa Turqish airline usiku wa manane. Wanyama akibeba CL hope tutamwona Uhuru akienda kumpokea airport.
Kwani Wanyama amekuwa mchezaji bora?
Ameongoza kwa ufungaji pale Spurs?
 
Hili jambo Linanikera sana mimi binafsi

Samatta amekuwa ndio kipenzi cha Serikali kwa wachezaji wanaopiga gozi nje ya nchi, anazungumzwa bungeni, anazungumzwa yeye peke yake ni Kama wanatengeneza picha kuwa ni yeye peke yake anayecheza huko ugaibuni wanasahau kuwa kwasasa wachezaji angalau wanaocheza nje ya nchi ni wengi tu sasa kumpongeza peke yake haifai

Najua kuwa samata anajitahidi kwa kiasi chake huko alipo lakini kuwekeza kwake peke yake sio picha nzuri

Jana nimemuona waziri mweye dhamana ya michezo akimpokea samata je ataenda kuwapokea na wengine?

Na waandishi wa habari walivyo sio watu wakujiongeza kila siku ubeligiji etiquette kwenda kumpongeza

Hili taifa letu nilaajabu ajabu hivi hadi nashindwa kuelewa

Kama mnatoa mailage kwa wachezaji wapeni heshima wote sio kuruka kuruka

Pale burundi kuna mchezaji anacheza uingereza ila huwezi kuona kelele Kama zinavyopigwa huku kwetu

Pale Kenya, Victor Wanyama anacheza uefa champions final lakini sioni wakenya wakipiga kelele km sisi

Uganda wanawachezaji huko ubeligiji lkn hawana kelele

Yaani sisi watanzania ni wakudeal na mambo madogo madogo tu

Mara wengine wanataka eti samata ajengewe sanamu ma waajabu haya!! Kwa lipi alilolifanya?

Serikali acheni kuendesha mambo kwa ushabiki wa mitandaoni.
wako wapi hao wengine???? Ninadhani kinachofanyika hivi sasa ni kuamsha chachu kwa wengine wafuate nyayo ili waende mbali zaidi ya samatta.
 
Waziri anaacha usingizi wake kwenda kumpokea Samata akishuka kwa Turqish airline usiku wa manane. Wanyama akibeba CL hope tutamwona Uhuru akienda kumpokea airport.
Raila Odinga akiwa PM alimsaidia Mariga kupata work permit ili aweze kusajiliwa na klabu ya England
 
Ninachomkubali Samatta mbali na sifa anazopewa yeye si mjivuni wala hana makuu.

Ni nahodha wa timu ya taifa pia anafanya vyema kimataifa kwahiyo anastahili hivyo wanavyomfanyia
 
Back
Top Bottom