Responded Wizara ya Michezo na TAMISEMI wako wapi wakati viwanja vya michezo na maeneo ya kijamii vikiendelea kubadilishiwa matumizi?

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Your browser is not able to display this video.
Kuna mambo ya kusikitisha, na mengine yanayoumiza. Ni matukio yanayokufanya ujiulize maswali mengi bila kupata majibu hasa ukiwaza mwelekeo kesho kwenye mambo muhimu yanayogusa ustawi wa jamii.

Mnamo Agosti 12, 2024, aliyekuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro, alifika eneo la Tegeta Wazo kufuatia malalamiko ya wananchi waliodai kuwa Uwanja wa Panga, uliokuwa ukitumika kwa shughuli za michezo na kijamii, ulikuwa umeanza kuchimbiwa mashimo ya msingi bila ushirikishwaji wa jamii husika.

Waziri alikutana na wananchi wa eneo hilo na kuafiki hoja zao, akieleza kuwa kilichokuwa kinafanyika kilikuwa kinyume na utaratibu. Aidha, alisema kuwa alikuwa ametumwa na Rais kufuatilia suala hilo.

Katika mazungumzo yake mbele ya kamera, Waziri alitoa saa 72 kwa wahusika waliokuwa wakichimba msingi waliodai kuwa walikuwa wakijenga shule, aliwataka kusitisha shughuli hizo, kusawazisha eneo lililochimbwa na kuurejesha uwanja katika hali yake ya awali ili uendelee kutumika kama ulivyokuwa.

Hata hivyo, baada ya agizo hilo, eneo hilo lilibaki na mashimo kwa zaidi ya miezi mitano bila maelekezo ya Waziri kutekelezwa. Baadaye, ilionekana mkandarasi akirejea na kuendelea na ujenzi kwa kasi huku eneo hilo likiwa chini ya ulinzi maalum wakati wote ambao ujenzi ulikuwa ukiendelea.

Kwa sasa, eneo lote la uwanja limejengwa. Vijana waliokuwa wakilitumia kwa mazoezi na michezo sasa wanahangaika kutafuta sehemu mbadala. Badala ya kuwaona uwanjani, mara nyingi unawakuta wakikaa vijiweni wakipiga soga au wakijihusisha na shughuli zisizo na tija katika muda ambao hapo awali walikuwa wakifanya mazoezi.


​
Wananchi tunajiuliza: Ni nani aliyekiuka maelekezo ya Waziri ambaye alisema kuwa alikuwa ametumwa na Rais? Kwa nini wananchi hawakusikilizwa ipasavyo kabla ya kufanyika kwa uamuzi unaoonekana kulazimishwa? Je, wahusika hawatambui kuwa hatua kama hizi zinaweza kuzalisha chuki na migogoro isiyo ya lazima?

Wizara ya Michezo na TAMISEMI wako wapi?
Hizi ni taasisi muhimu zenye wajibu wa kulinda na kuendeleza maeneo ya michezo na shughuli za kijamii. Hata hivyo, zinaonekana kuwa kimya wakati maeneo mengi ya wazi, ikiwemo viwanja vya michezo na vile vilivyokuwa vikitumika kwa shughuli za kijamii, vinaendelea kubadilishiwa matumizi bila kuwepo kwa maeneo mbadala kwa jamii.

Mfano mwingine

Kwa sasa, viwanja kama Biafra (Kinondoni), Sahara (Mabibo-Ubungo) na Uwanja wa Kiwalani Hospitali, miongoni mwa vingine, tayari vimeanza kutumika kwa shughuli tofauti bila ushirikishwaji wa wananchi. Hata kama viwanja hivyo vinamilikiwa na taasisi mbalimbali, vimekuwa sehemu muhimu ya historia na ustawi wa jamii. Kwa hiyo, mabadiliko yoyote ya matumizi yanapaswa kufanyika kwa uwazi na kwa kushirikisha wananchi.
​
Wito wa uwajibikaji
Natoa wito kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) kufuatilia michakato ya kubadili matumizi ya viwanja vya wazi pamoja na viwanja vya michezo ili kuhakikisha sheria na taratibu zinafuatwa.

Vilevile, wito wangu mwingi kwa Serikali kuweka mkakati wa wazi wa kulinda maeneo ya wazi, hususan viwanja vya michezo, ambavyo vina mchango mkubwa katika maendeleo ya kijamii, afya na malezi ya vijana.

Aidha, natoa wito kwa wadau wote wenye umiliki wa viwanja ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa vikitumika kwa shughuli muhimu za kijamii ikiwemo viwanja vinavyomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba kabla ya kufanya maamuzi ya kuviendeleza kwa matumizi mengine, ni muhimu kuzingatia maslahi ya umma na kushirikisha jamii inayovitumia ili kuepuka migogoro ya kijamii.

Pia soma ~
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kaspar Mmuya apiga marufuku uvamizi wa maeneo ya wazi
 
[16/06, 11:25] Lunele .com🌳: Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Samia ina aleji kubwa na miradi ya kimkakati iliyoanzishwa kwa lengo la kumaliza matatizo ya watanzania.

Rais Samia amegoma kuuzindua mradi wa bwawa la Nyerere uliojengwa kwa lengo la kukomesha tatizo la umeme ndani ya nchi.

Rais Samia amegoma kuzindua barabara ya njia nane kutoka kimara hadi Kibaha uliojengwa kwa ajili ya kukomesha tatizo la foleni jijini.

Rais Samia amegoma kuipa msukumo bandari kavu ya kwala ili ijae makontena yatakayozuia foleni malori kuingia jijini na kuongeza foleni lakini pia kuharibu barabara za mitaa vibaya sana. Kila kona ya jiji sasa hivi wanajenga ICD za kuhifadhi makontena!

Rais Samia amegoma kuupa uzito mradi wa reli ya SGR hali iliyopelekea kipande cha Mwanza mkandarasi kufukuza wafanyakazi na kusuasua sana.

Serikali ya Samia haijulikani ni nini na iko uchumi gani maana uchumi wa kati tulishatolewa!

Serikali ya Samia yatenga Tzs trillion 1 kwa ajili ya safari.



Inasikitisha sana
[16/06, 11:29] Ngeme Voda: Halotel wapi?
 
Wakimaliza huko watakuja kupora maeneo ambayo ni ya raia..
Mlafi hana kikomo
Kabisa ndiko tunakokwenda hko
Jiji au mkoa utakosaje kuwa na maeneo ya wazi
Hivi hawa viongozi hawaoni aibu
Sema wakubwa huko juu ni magumashi mtu kuanzia wakurugnzi wa jiji,mameya, madiwani nk
Tunajuwa watoto zao wao wanawapeleka kwenye viwanja vya kulipia!

Hapa nawaza tu ule uwanja wa magunia msasani sijuwi kama utapona najuwa kuna watu wanaupigia hesabu
Hao hao mbogamboga

Ova
 
Hauwezi kupona, we tizama tu pale ulipo, msasani ni dili kubwa sana, sijapita huko muda imani yangu ikawa inaniambia kwa speed hii huenda nao ushabebwa.
 
Hauwezi kupona, we tizama tu pale ulipo, msasani ni dili kubwa sana, sijapita huko muda imani yangu ikawa inaniambia kwa speed hii huenda nao ushabebwa.
Biafra uwanja nmemuliza diwani kimya, watu fulani kimya
Ila tatizo linakuja pale utasikia maeneo haya ni ccm
Hata mm muda sijapita hapo uwanja magunia ila kwa jinsi eneo lilivyo sjui kama litapona

Ova
 
Hauwezi kupona, we tizama tu pale ulipo, msasani ni dili kubwa sana, sijapita huko muda imani yangu ikawa inaniambia kwa speed hii huenda nao ushabebwa.
Mimi mkazi wa kinondoni nyuma ya mango, mafele
Pale kuna uwanja miaka nenda rudi watu wamekuwa wakaitumia mazoezi kufanya,kuna wakati pale walimwaga vifusi mbona waliviondoa,
Kdg watu pale wana msimamo ila wangelegea ilikuwa byebye

Ova
 
Mimi mkazi wa kinondoni nyuma ya mango, mafele
Pale kuna uwanja miaka nenda rudi watu wamekuwa wakaitumia mazoezi kufanya,kuna wakati pale walimwaga vifusi mbona waliviondoa,
Kdg watu pale wana msimamo ila wangelegea ilikuwa byebye

Ova
Kwenye jamii ambayo mbwa mwitu ndio mtunga sheria, swala ajue hana chake.
 
Biafra uwanja nmemuliza diwani kimya, watu fulani kimya
Ila tatizo linakuja pale utasikia maeneo haya ni ccm
Hata mm muda sijapita hapo uwanja magunia ila kwa jinsi eneo lilivyo sjui kama litapona

Ova
Kupona ni ngumu sana mzee baba.
 
Hii hali ndio inachangia vijana kuingia kwenye madawa, kinondoni wamepora viwanja vingi na haya ndio matokeo yake
 
Serikali haina hela wala wafadhiri, inakusanya pesa kwa wawekezaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…