Wizara ya Nishati yalaumiwa kumkwamisha mwekezaji umeme wa upepo Singida

Wizara ya Nishati yalaumiwa kumkwamisha mwekezaji umeme wa upepo Singida

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Elia Digha ameilaumu Wizara ya nishati kwa kumkwamisha mwekezaji anayetaka kuzalisha umeme kwa njia ya upepo mkoani Singida.

"Nimezungumza nao wawekezaji wanasema wanakwamishwa na wizara husika, watu wasikwamishe miradi ambayo iko wazi Rais anahangaika kutafuta wawekezaji

 
Hajawapa chao
Nchi ya hovyo sana
Usimsahau pia, huyo mwenyekiti anaweza kuwa tayari kapata fungu lake..., kwa upande wa pili!

Ndivyo nchi inavyokwenda sasa, kila mtu kwa "urefu wa kamba yake."
 
Usimsahau pia, huyo mwenyekiti anaweza kuwa tayari kapata fungu lake..., kwa upande wa pili!

Ndivyo nchi inavyokwenda sasa, kila mtu kwa "urefu wa kamba yake."
Mwenyekiti kapata fungu wapi tena?
 
Mambo usiyoyajua ni sawa na usiku wa giza. Umeme wa upepo na jua kuunganisha kwenye grid sio rahisi kama watu wanavyodhani, unaweza kusababisha matatizo mkubwa.
 
Mambo usiyoyajua ni sawa na usiku wa giza. Umeme wa upepo na jua kuunganisha kwenye grid sio rahisi kama watu wanavyodhani, unaweza kusababisha matatizo mkubwa.

Mawazo mugando na ushamba tu huo. Matatizo makubwa?!! You’re not serious.
 
Ugatuzi - sera ya kupeleka mamlaka ya baadhi ya maamuzi yafanywe ktk ngazi ya mikoa / majimbo bila kusubiri siasa za wizara / bunge za huko Dodoma au Dar es Salaam inafaa kuanza kutumika na kutiwa ndani ya katiba mpya.

Masuala ya uchimbaji visima vya maji, kuzalisha umeme uwe wa upepo au maporomoko madogo ya maji yasihitaji mpaka serikali kuu kuingilia utekelezaji. Serikali kuu Dodoma na Dar es Salaam intengeneze sera tu ya nchi kuhusu umeme na vyanzo vyake utekelezaji uachiwe mikoa / majimbo.
 
TOKA MAKTABA:

2 November 2016
Bunge, Dodoma

Je, serikali itakamilisha lini mradi wa umeme wa upepo mkoani Singida? hapa naibu waziri Mhe. Medard Kalemani

Dr. Medard Kelemani bungeni 2016 alielezea mkakati kuhusu umeme wa upepo Singida kuwa utakamilika April 2019.




More info :

08 December 2016​

Dar es Salaam, Tanzania

WANANCHI WA SINGIDA KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME WA UPEPO​


DSC_0095
DSC_0118
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba akizungumza leo December 2016 kwenye mkutano wa wadau wa umeme kujadili mkakati ya kuzalisha nishati ya Umeme kwa njia ya Upepo leo katika ukumbi wa Hotel ya Hyatt Jijini Dar
DSC_0137 Mkurugenzi Mtendaji Six Telecoms, Rashid Shamte (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye kongamano la wadau wa umeme wenye lengo la kuzalisha umeme wa nguvu ya Upepo wenye lengo la kuanza kuzalisha umeme katika mkoa wa Singida.

DSC_0103
DSC_0104
Baadhi ya wadau wakiwa kwenye kongamno la wadau wa umeme
DSC_0183
DSC_0194
Mkurugenzi Mtendaji Six Telecoms, Rashid Shamte akizungumzia uzalishaji wa umeme kwa njia ya upepo utakaosimamiwa na Kampuni ya kuzalisha umeme huo ya Afrika Masharikana awamu ya kwanza itaanzia mkoani Singida.
DSC_0187
Alex Moulds kutoka Energy Net Limited akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuzalisha umeme wa Upepo

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mh. January Makamba amesema kuwa mpango wa serikali ni kuwa na vyanzo vingi vya uzalishaji umeme ili kuwa na vyanzo vya nchi endelevu na kuunga mkono juhudi za benki ya dunia kuzalisha umeme wa upepo katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

Makamba amesema hayo wakati wa Kongamano la wadau wa Nishati ya umeme walipokutana kuzungumzia matumizi ya Nishati ya umeme inayozalishwa kwa njia ya upepo itakayounganishwa kwenye gridi ya taifa na mfumo huo utawasaidia wananchi wa Singida .

"Kwa kuwa umeme huo utazalishwa kwenye maeneo ya vijijini, wananchi wanatakiwa kupata umeme kwa bei rahisi kulingana na uchumi wao na sio kuuziwa umeme kwa bei juu, na zaidi Wizara yake inapenda kuweka wazi kuwa huu mradi una faida kubwa sana kulingana na mfumo wa nchi ulivyo,"amesema Makamba.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha umeme wa upepo Afrika Mashariki Six Telecoms, Rashid Shamte amessema kuwa mfumo huu wa gridi ndogondogo una faida kubwa sana kwa wananchi kwani asilimia kubwa kulingana na ripoti ya benki ya dunia wananunua umeme wa bei nafuu kwahiyo serikali imekubaliana na kampuni yetu na imeweza kukubali kuwa mradi huu una tija na utasimamiwa na serikali yenyewe kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida pamoja na Halmashauri.

Shamte ameendelea na kusema, kwa Phase ya kwanza watatoa umeme megawati 100 na itaendelea mpaka kufika megawati 300 na wataunganisha kwenye gridi ya taifa, na huu mradi utakuwa na faida kwa wananchi pamoja na wale watakaotolewa kwenye maeneo yao watafaidika kwa kulipa stahiki zao.

Kwa upande wa Wizara ya Nishati na Madini, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo amewataka wawekezaji hao kuuza umeme kwa bei rahisi kwani mara nyingi mipango ya serikali imekuwa haiendani na mikakati ya wawekezaji kwahiyo wanategemea kuona kuwa mradi huu uwe nafuu ya wananchi wa vijijini kupata umeme kwa bei rahisi.
 
ADSW Summit: Interview: Using Green Energy to Unlock Africa’s Enormous
24 January 2022



Speakers: H.E. January Makamba, Minister of Energy, Tanzania on Energy Mix
Moderator: Eithne Treanor, Managing Director, E Treanor Media, United Arab Emirates
 
Mawazo mugando na ushamba tu huo. Matatizo makubwa?!! You’re not serious.
Dah! Ndio maana serikali hua hapotezi muda kujibu, wanakataa tu kimyakimya. 🤣🤣

Ni mambo ya kitaalamu hayaelezeki kirahisi rahisi kwa mtu asiye na A wala B kwenye fani hiyo.
 
Hapa kuna jambo ...six telecom imefilisiwa kudaiwa kodi na TRA huyo Shante na Directors wake Mzee Nobi na Dr Tanga wanekaa sana jela....hiyo kampuni hapo tena labda wawekezaji wapya waje ...
 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Elia Digha ameilaumu Wizara ya nishati kwa kumkwamisha mwekezaji anayetaka kuzalisha umeme kwa njia ya upepo mkoani Singida.

"Nimezungumza nao wawekezaji wanasema wanakwamishwa na wizara husika, watu wasikwamishe miradi ambayo iko wazi Rais anahangaika kutafuta wawekezaji
Tatizo hapa linaweza kuwa kwenye makubaliano ya kuuza umeme. Mtakumbuka ile mikataba ya Kikwetena kampuni ya mfukoni ambayo iliiba matrillioni na kuwafanya wahusika wa mwisho kukaandani miaka. Haya makampuni yanakuwaga na vipengele ambavyo wataendelea kuvuna hata kama hawatoi huduma. Ile kampuni ya mwanzo utumieumeme usitumie unalipa. Mitamboikisimama hata kwa ajili ya service unalipa. Huyu muwekezaji wa Singida anakwamishwa kumbe kuna kutokuelewana kwenye mkataba. Kwa hiyi tusilichukulie hili la kukwamishwa kama kweli nikukwamishwa, huenda kuna vipengele kwenye mkataba ambavyovikikubalika tutakuwa tumuingizwa choocha kike.
 
Ugatuzi sera ya mkio / majimbo kuweza kutekeleza miradi dizaini hii bila kusubiri siasa za wizara / bunge huko Dodoma au Dar es Salaam .

Masuala ya uchimbaji visima vya maji, kuzalisha umeme uwe wa upepo au maporomoko madogo ya maji yasihitaji mpaka serikali kuu kuingilia utekelezaji. Serikali kuu Dodoma na Dar es Salaam intengeneze sera tu ya nchi kuhusu umeme na vyanzo vyake utekelezaji uachiwe mikoa / majimbo.
Sure kusubiri serikali kuu iamue kila kitu nao ni kuchelewesha maendeleo tuu
 
Back
Top Bottom