WIZARA YA NISHATI YASHIRIKI TAMASHA LA KIZIMKAZI ZANZIBAR
📌 Yatoa huduma moja kwa moja kwa Wananchi kupitia Taasisi zake
📌 Nishati safi ya kupikia, yawa ajenda ya kuvutia
Zanzibar.
Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zake leo Agosti 21, 2024 zimeshiriki katika Tamasha la Kizimkazi (Kizimkazi Festival) yanayoendelea kwenye kijiji cha kizimkazi wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini Kisiwani Zanzibar.
Katika tamasha hilo la Kizimkazi Wizara na taasisi zinatoa elimu ya utekelezaji wa Sera ya Nishati ya mwaka 2015 pamoja na kutoa huduma kwa wananchi hususani katila utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa mwaka 2024-2034.
Katika Banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wananchi wameweza kujionea moja kwa moja shughuli za uchimbaji wa Gesi Asilia, usafirishaji na uchakataji wake kupitia teknolojia ya Uhalisia Pepe ( Virtual Reality) pamoja na kuelezwa juhudi za Serikali katika uendelezaji wa Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia.