Wizara ya Sanaa na Michezo: Pamba Jiji FC kufanya mazoezi gizani ni kwa sababu hawakutoa taarifa mapema

Wizara ya Sanaa na Michezo: Pamba Jiji FC kufanya mazoezi gizani ni kwa sababu hawakutoa taarifa mapema

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imekanusha madai yaliyoenea mitandaoni kuwa timu ya Pamba Jiji FC ilifanya mazoezi gizani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa Septemba 23, 2025, wizara imesema timu hiyo iliingia uwanjani bila taarifa rasmi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Yanga SC unaotarajiwa kuchezwa kesho Septemba 24, 2025.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, wachezaji wa Pamba Jiji waliwasili uwanjani majira ya saa 12:35 jioni wakati wataalamu wa umeme walikuwa wamemaliza kazi na kuondoka, hivyo taa ziliwashwa tena saa 1:08 usiku.


Aidha, wizara imeeleza kuwa video zinazosambaa zikionesha wachezaji wakifanya mazoezi gizani si sahihi, kwani chanzo chake ni uchelewaji wa kufika uwanjani. Wizara pia imeitaka timu zinazotumia uwanja huo kufuata utaratibu wa kuomba kibali mapema ili kuepusha usumbufu.

bagram.png
 
Kimbelembele chao hao Pamba. Viwanja vipo vingi kwani ilikuwa lazima waende hapo.

Huo sio uwanja mgeni kwao.
 
Halafu mnashangaa Yanga huwa wanapitia milango isiyoruhusiwa kuingia uwanjani kwenye crucial games sasa unapata majibu funguo zinatoka wapi za kufungua hiyo milango. Timu zingine wanasema hawatoi taarifa je Yanga huwa wanamwambia nani?
 
Kanuni zipo wazi,timu itakuja kufanya mazoezi ya mwisho siku moja kabla ya mechi muda sawa na ule mechi itachezwa!

Taarifa gani tena wapewe kama timu imefika ndani ya muda?

Hilo geti limefunguliwaje sasa kama hakuna taarifa maana Simba wao walizuiwa kuingia tukaambiwa hawakutoa taarifa!

Hawajui kama kuna mechi kesho au hawajui muda wa mechi?

Hizi negligence ndiyo zilipelekea CAF kuufungia uwanja msimu uliopita,usimamizi wa huo uwanja umejaa siasa za bei ya jioni!!
 
Mimi nafkiri kuhusu hilo swala la taa ni kutofautiana ratiba tu kati ya uongozi wa uwanja na timu ya pamba, lakini siamini kabisa kama yanga wamehusika kama ambavyo baadhi ya watu wanataka kuaminisha umma
 
Simba yeye last-born anacheza lini? Au anapumuzishwa ili kushiriki vema michuano ya kimataifa?
 
Wizara yenye dhamana na michezo imeshatolea ufafanuzi! Cha kushangaza bado kuna watu wanajitahidi kuona Yanga inahusishwa kwa namna yoyote ile! Jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo.
 
Wizara yenye dhamana na michezo imeshatolea ufafanuzi! Cha kushangaza bado kuna watu wanajitahidi kuona Yanga inahusishwa kwa namna yoyote ile! Jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo.
Ficha upumbavu wako basi. Pamba haichezi na Wizara au Wizara Wana timu Ligi Kuu? Yanga ndio anapaswa kujua timu pinzani inapata uwanja wa mazoezi na mazingira rafiki.
 
Ficha upumbavu wako basi. Pamba haichezi na Wizara au Wizara Wana timu Ligi Kuu? Yanga ndio anapaswa kujua timu pinzani inapata uwanja wa mazoezi na mazingira rafiki.
Kuna baadhi ya viumbe mkiwa kwenye siku zenu huwa mnawashwawashwa tu kutukana watu.
 
Back
Top Bottom