DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Kufuatia taarifa zinazosambazwa mitandaoni kuhusu picha jongevu mbalimbali za ukiukwaji wa maadili ya Mtanzania zikionesha baadhi ya watu wakicheza ngoma na aina nyingine za muziki zisizo na staha katika maeneo ya wazi, vyombo vya usafiri na makazi, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inalaani vikali vitendo hivyo vinavyokiuka misingi ya maadili ya Mtanzania na kuleta taharuki kwenye jamii.
Wizara inatoa wito kwa wadau wote wenye taarifa za kuwapo kwa matukio ya uvunjifu wa maadili, kutoa taarifa katika mamlaka zinazohusika ikiwemo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Jeshi la Polisi ili wahusika wachukuliwe hatua mara moja kwa mujibu wa sheria kama ambavyo wamekuwa wakichukuliwa hatua wengine.
Hata hivyo, Wizara inatoa wito kwa wadau wanaoona ama kubaini maudhui ya ukiukwaji wa maadili, kujiepusha kuyasambaza mitandaoni kwa kuwa usambazaji wa maudhui hayo unasababisha madhara zaidi kwa jamii na pia ni ukiukwaji wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 inayokataza usambazaji wa picha zisizo na maadili kwa jamii. Hivyo, wahusika wanaoendelea kusambaza picha hizo ikiwemo kuzichapisha kwenye mitandao ya kijamii wanaelekezwa kuzifuta mara moja ili kulinda maadili ya Kitanzania na kujiepusha na makosa ya kimtandao.
Wizara inatoa rai kwa jamii kama ilivyobainishwa katika Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 kuwa, suala la usimamizi wa maadili ya Mtanzania ni jukumu la jamii nzima. Aidha, Wizara inaendelea kushirikiana na wadau kutoa elimu kwa makundi mbalimbali na kuchukua hatua kwa wale wote wanaokiuka misingi ya maadili ya Mtanzania kwa makusudi.