Wizara ya uchukuzi na kampuni kikorea matatani, madeni yawaandama

Wizara ya uchukuzi na kampuni kikorea matatani, madeni yawaandama

Nyanswe Nsame

Senior Member
Joined
Jul 9, 2019
Posts
165
Reaction score
181
WIZARA YA UCHUKUZI, KAMPUNI YA KICHINA MATATANI, MADENI YAWAANDAMA

WIZARA ya Uchukuzi kwa kushirikiana na kampuni ya KICHINA ya China Railway 15 Bureau Group corporation (CR15G) inatuhumiwa kuvunja mkataba na kampuni ya AQARIAN Project Solutions walioingia kujenga na upanuzi gati (kina).

Kampuni hiyo ya KICHINA iliingia mkataba na kampuni ya kizawa ya AQARIAN Project Solutions kujega na kuongeza kina kwa kiasi cha zaidi ya shilingi 290.

Baada ya kampuni hiyo kufanya kazi kwa miezi tisa, hata hivyo mkataba ulivunjwa baada ya Kampuni hiyo ya kichina kushindwa kuilipa kampuni ya kizawa bila sababu zozote za msingi.

Tangu kampuni hiyo ya kizawa ianze ujenzi wake ililipwa kiasi kisichozidi milioni 30 pekee na baadhi ya kazi zilizokuwa zimefanywa na kampuni hiyo fedha zake hazijalipwa.

Baada ya kuvunja mkataba huo na kampuni ya kizawa iliyokuwa na jukumu la kuongeza na kupanua kina ziwa Victoria katika bandari ya Mwanza kasikazini walianza kuwatumia vijana wa mtaani wasiokuwa wataalamu.

Vijana wanaotumiwa na kampuni hiyo ya kichina chini ya usimamizi wa Mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini TPA, vijana hao wengi wao sio watalamu mara nyingi husomba mawe kwa mikono kurusha kwenye maji kutengeneza kina hicho.

Kitendo hicho cha kutumia vijana hao ambao sio wataalamu kilisababisha mmoja wa kijana kupoteza maisha baada ya kuzama ziwa Victoria.

Ipo hivi, baada ya kuvunjwa kwa mkataba, kampuni hiyo ya kizalendo imeandika barua Februari 12, 2024 ikielezea namna TPA ilivyoshiriki njama za kuvunja mkataba ili kutengeneza mazingira ya upigaji wa fedha ambazo ingelipwa kampuni hiyo.

Barua ya kampuni hiyo ya kizalendo imeeleza na kutaja kiasi cha shilingi milioni 47, 082,000.00 ambacho inaomba kulipwa Kama fidia baada ya kuvunjiwa mkataba na mambo mengi.

Kampuni ya AQARIAN Project Solutions inaeleza kwamba endapo kampuni hiyo ya kichina itashindwa kulipa kiasi hicho cha fedha itachukua hatua ya kuifikisha mahakamani ikiiunganisha na Serikali kwa kushindwa kusimamia haki za watanzania.

Pia kampuni hiyo nje ya madai hayo,Novemba 27 2023 iliingia mkataba mwingine na kampuni hiyo ya kichina, kuwa mhandisi mkuu wa kusimamia ujenzi wa upanuzi wa gati ambalo litatumika kutia nanga meli ya MV Mwanza ambako pia mkataba umevunjwa.

Kampuni ya AQARIAN Project Solutions ilishinda tenda namba AE/016/2022-23/HQ/W/I0 na ilifanya kazi kwa miezi tisa bila kulipwa na makubaliano yalikuwa kwa mwezi ni shilingi milioni tatu.

Kufuatia kuwepo kwa mkanganyiko huo, AQARIAN Project Solutions iliandika barua Agousti 29, 2024 ya kuvunja mkataba ikiomba kulipwa shilingi milioni 27,000,000 na fidia ya milioni 10.

Baada ya barua ya kampuni hiyo kizalendo, ambapo Septemba 2, mwaka huo huo, China Railway 15 Bureau Group corporation (CR15G) walijibu barua hiyo ikionesha kufahamu jambo hilo.

Chanzo cha ndani ya kampuni hiyo ya kichina kinaeleza kuwa walivunja mkataba na kampuni hiyo ya kizawa na kushindwa kuilipa fedha zake baada ya vigogo wa TPA kulazimisha fedha hizo zipite kwenye kampuni nyingine iliyopewa kazi bila kutangazwa kwa zabuni.

Kampuni ya AQARIAN Project Solutions inakusudia kwenda mahakamani kudai haki zake kutokana na kuingia mikataba hiyo miwili na kushindwa kulipwa fedha zake.

NB: Picha na VIDEO vijana wakiwa kazini, hawana Vifaa maalamu vya mahala pa kazi.

86e16df9-d3ff-48b1-93e0-1062fd74acfa.jpeg
7bfde276-8ba9-4273-a8d4-488f4289b5f6.jpeg
9fee50ce-58b7-4cd0-8f7b-2395e521c245.jpeg

 
Mchina hio kampuni aliifungulia Korea 🐗🐗 hio hela watu wa kula kwa urefu wa kamba zao walishapita nayo
 
Back
Top Bottom