BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Katika mwaka wa fedha 2024/25, Wizara ya Ujenzi inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 1,769,296,152,000 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Kati ya fedha hizo Shilingi 81,407,438,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ya Wizara na Taasisi na Shilingi 1,687,888,714,000 kwa ajili
ya Miradi ya Maendeleo.
Kati ya fedha za Matumizi ya Kawaida, Shilingi 76,588,233,000 ni za Mishahara ya Watumishi na Shilingi 4,819,205,000
ni za Matumizi Mengineyo.
Bajeti ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inajumuisha fedha za ndani Shilingi 1,141,803,989,000 na fedha za nje ni Shilingi 546,084,725,000 Fedha za ndani zinajumuisha Shilingi 599,756,467,800 kutoka Mfuko wa Barabara na Shilingi 542,047,521,200 ni fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali.
WIZARA YA UJENZI YAOMBA BAJETI YA TRILIONI 1.77
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewasilisha makadirio ya bajeti ya shilingi trilioni 1.77 kwa ajili ya utekelezaji vipaumbele tisa vyenye miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja, vivuko, mizani, ukamilishaji viwanja vikubwa vya ndege.
Amesema kati ya kiasi hicho cha fedha, sh. bilioni 81.4 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. Trilioni 1.6 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Hayo aliyasema bungeni jana wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25 ambapo alisema katika mwaka huo wa fedha, Wizara inatarajia kutekeleza Mpango na Bajeti kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26).
Aidha, Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020, Mpango Mkakati wa Wizara (2021/22 – 2025/26), Ahadi za Viongozi Wakuu wa Serikali na Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Bashungwa alisema Wizara imeandaa Makadirio ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 kwa kuzingatia vipaumbele 9.