Wizara ya Ujenzi yaomba Trilioni 2.5 kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

Wizara ya Ujenzi yaomba Trilioni 2.5 kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega (Mb.), akiwasilisha Bungeni Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya fedha kwa mwaka wa Fedha 2026/27 ya Wizara ya Ujenzi leo, tarehe 20 Mei 2026,
amesema kuwa jumla ya Tsh 2,564,441,414,000 zinahitajika ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya wizara pamoja na taasisi zilizo chini yake kwa mwaka ujao wa fedha.

Mchanganuo wa Matumizi ya Kawaida na Miradi

Miradi ya Maendeleo
: Jumla ya Tsh 2,467,336,479,000 (zaidi ya bilioni 2,467) zimetengwa mahususi kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali ya kitaifa.

Matumizi ya Kawaida: Jumla ya Tsh 97,104,935,000 zitaenda kwenye matumizi ya kawaida ya wizara na taasisi zake, ambapo Tsh 92,209,218,000 ni kwa ajili ya mishahara na Tsh 4,895,710,000 kwa ajili ya matumizi mengineyo

Vyanzo vya Fedha za Maendeleo
Akigusia upatikanaji wa fedha za miradi ya maendeleo, Waziri Ulega amebainisha kuwa serikali itaendelea kutumia vyanzo vya ndani na ushirikiano wa wadau wa maendeleo wa nje:

Fedha za Ndani: Shilingi trilioni 1.54 (Tsh 1,544,872,140,000).

Fedha za Nje (Wadau): Shilingi bilioni 922.46 (Tsh 922,464,330,000).


 
Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amewasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2026/2027 leo Jumatano tarehe 20 Mei, 2026 , ambapo Wizara hiyo imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 2,564,441,414,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Akiwasilisha makadirio hayo leo Jumatano Mei 20, 2026 mbele ya Bunge la Tanzania jijini Dodoma, Waziri Ulega amesema bajeti hiyo inalenga kuimarisha utekelezaji wa miradi ya miundombinu nchini, hususan sekta ya barabara.

Kwa mujibu wa mapendekezo hayo ya bajeti, kati ya Shilingi 2,564,441,414,000 zilizoombwa, Shilingi 97,104,935,000 zimetengwa kwa matumizi ya kawaida ya Wizara na taasisi zake, huku Shilingi 2,467,336,479,000 zikiwa ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Aidha, kati ya fedha za matumizi ya kawaida, Shilingi 92,209,218,000 zimetengwa kwa ajili ya mishahara ya watumishi, na Shilingi 4,895,717,000 zikiwa ni kwa ajili ya matumizi mengineyo ya uendeshaji wa shughuli za kila siku.

Kwa upande wa bajeti ya maendeleo, fedha za ndani zimepangwa kuwa Shilingi 1,544,872,147,000, wakati fedha za nje ni Shilingi 922,464,332,000. Fedha za ndani zinajumuisha Shilingi 1,047,405,500,000 kutoka Mfuko wa Barabara na Shilingi 497,466,647,000 kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali.

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi imeeleza kuwa fedha hizo zitatumika katika ujenzi, ukarabati na uboreshaji wa miundombinu ya barabara nchini ili kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi.
 
Yanavimba mishavu tu kutaja hela yaibe,sasa hivi tu mbeya wametoka kulalamika pale mwanjelwa barabara 4 haikamiliki.
Huku mtu anataka tilioni 2+
 
Back
Top Bottom