Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa yaomba Tsh Trilioni 4.2 kutekeleza majukumu ya Wizara mwaka wa fedha 2026/2027

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa yaomba Tsh Trilioni 4.2 kutekeleza majukumu ya Wizara mwaka wa fedha 2026/2027

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imeomba Bunge kuidhinisha jumla ya shilingi trilioni 4.2 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo kwa Mwaka wa Fedha wa 2026/2027.

Akiwasilisha makadirio hayo ya bajeti bungeni jijini Dodoma leo, Jumanne, Mei 19, 2026, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Rhimo Nyansaho, amebainisha mchanganuo wa fedha hizo mbele ya Bunge

Katika hotuba yake, Waziri Nyansaho amesema kuwa kati ya kiasi hicho kilichoombwa, shilingi trilioni 3.85 zitatumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya wizara na taasisi zilizo chini yake. Kiasi kilichosalia, ambacho ni shilingi bilioni 426.58, kimetengwa rasmi kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ya jeshi.

"Kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na taasisi zilizo chini yake inaliomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya shilingi trilioni nne, bilioni mia mbili themanini na sita, milioni mia nne themanini na tisa na laki moja na kumi na tano (4,286,489,115), ambazo kati ya fedha hizo, shilingi trilioni tatu, bilioni mia nane hamsini na tisa, milioni mia tisa hamsini na tano na laki nne na sitini na mbili (3,859,955,462) ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni mia nne ishirini na sita, milioni mia tano themanini na tatu, laki sita na hamsini na tatu (426,583,653) ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo."

"
 
Kodi ya watanzania inaibiwa kila kona. Ni pesa isiyo na mwenyewe.
 
Back
Top Bottom