Wizara ya Utalii mnatia aibu

Wizara ya Utalii mnatia aibu

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Hivi unaweza kuamini hadi tarehe ya leo

Kuna kituo kimoja tu cha kuchukua sample za Korona kwenye Mbuga zote Tanzania. Wenzetu Kenya ka mbuga kadogo ( Masai Mara) kama robo ya Serengeti kanavyo zaidi ya 10 yaani jamani haingii akilini!!

Hicho Kituo kimoja cha Seronera ni private sector wameweka na TANAPA wakachangia kama robo kwa kuweka vitu ambavyo hakiwa hata vya kipaumbele kama TV ambayo hata wageni hawana muda wakuitizama.

Imagine: Sasa nyumbu wana elekea North Serengeti hakuna hata kituo kimoja; wakati gharama yake ni kama shs 10 - 15 mil ambapo naamini kabisa private sector wapo tayari kutoa malazi ya wataalamu bure kabisa.

Ila ukiuliza kwetu unaweza kutajiwa 40mil kwa kituo, yaani mtu anapropose sola ya 5mil + utafikiri anaendesha kiwanda cha mikate (kwetu kila kitu ni deal). Wageni wanahitaji simple tent moja ya kuchukua sample na fly sheet ya kujiandikisha BASI.

Ngorongoro hadi msimu umeisha wameshindwa kuweka hata kituo kimoja pale Ndutu; halafu wanalialia watalii wamepungua; Shame!
Kuwasaidia tu Ngoro ngoro wanahitaji vituo viwili tu (Headquarter na kingine Ndutu).

Serengeti wanahitaji kwa kuanzia walau vinne Kimoja kipo, hivyo bado ( Grumeti - western), Kogatende - North) na Lobo - East) with immediate effect. Unaweza kushtukia Wanafungua kituo North Serengeti November wakati nyumbu wanaondoka ( Shame!!!

Park za kusini ndio zimetelekezwa kabisa Ruaha, Nyerere NP, Katavi, Mahale. Zaidi tu utasikia tunapandisha tozo wakati watalii wenyewe tunawakimbiza kwa kuto meet mahitaji ya utalii kwa sasa HAPO UTASIKIA TUPO KWENYE UCHAMBUZI YAKINIFU HADI MSIMU UNAISHA!

Saa nyingine nashindwa kumlaumu mbunge Msukuma kwa hawa wasomi wetu
 
Umeongea ki professional sanaaa bro heko
 
sasa ndugu kwa maisha ya mwendazake yule aliyekuwa haamini juu ya uwwpo wa corona wala mqtumuzi ya barakoa, ni kiongozi gani angediriki kushauri haya uyawazayo?? kwa sasa kulingana na mtizamo wa mama naimani mambo mengi yatakaa sawa
 
sasa ndugu kwa maisha ya mwendazake yule aliyekuwa haamini juu ya uwwpo wa corona wala mqtumuzi ya barakoa, ni kiongozi gani angediriki kushauri haya uyawazayo?? kwa sasa kulingana na mtizamo wa mama naimani mambo mengi yatakaa sawa

Nadhani uelewa ndio tatizo hapa, mwendazake hakuamini korona kuwa ipo Tz lakini sio duniani huko na watalii wengi ni wa kutoka mataifa mengine duniani. Na ndio maana aliweka vituo vya kupima korona. Sio kila kitu kumsingizia mwendazake jamani
 
Back
Top Bottom