Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Dkt. Joel Nanauka leo Aprili 20, 2026 atawasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma.
Aidha, kabla ya bajeti hiyo kuwasilishwa, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, itawasilisha randama za makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ambapo kesho Aprili 21, 2026 bajeti ya wizara hiyo itawasilishwa bungeni.
Mbali na hayo, kutakuwa na kipindi cha maswali na majibu ambapo Wabunge watapata nafasi ya kuuliza maswali kwa Serikali.
Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 zinaonyesha kuwa Tanzania Bara ina jumla ya vijana 20,612,566 wenye umri wa miaka 15 hadi 35, ambayo ni sawa na 34.4% ya idadi ya watu wote. Aidha, kwa mujibu wa utafiti wa nguvu kazi kwa mwaka 2020/2021, vijana wanachangia zaidi ya 55% ya nguvu kazi ya Taifa.
Takwimu hizi zinaonyesha wazi kuwa vijana ndiyo sehemu kubwa zaidi ya nguvu kazi inayoshiriki katika shughuli za kiuchumi nchini. Hivyo, maendeleo ya vijana yanahusiana moja kwa moja na tija ya uzalishaji, ukuaji wa sekta mbalimbali za uchumi, pamoja na uwezo wa Taifa katika kuzalisha mali na huduma.
Ukweli usiopingika kuwa pamoja na ukubwa wa nguvu kazi ya vijana iliyopo nchini, nguvu kazi hii imeendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali kama ifuatavyo:
Ukosefu wa ajira: Ambapo kwa mujibu wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2021, vijana wameendelea kukabiliwa na ukosefu wa ajira kwa 12.2% (wanaume ikiwa ni 8.1% na wanawake 16.1%).
Upungufu wa ujuzi: Nguvu kazi iliyopo ina upungufu wa ujuzi wa mahitaji ya soko la ajira kwa kiwango cha chini, ambapo ni 76.9% badala ya 54% inayotakiwa; kiwango cha kati ni 19.9% badala ya 34%; na kiwango cha juu ni 3.2% badala ya 12% kwenye nchi zenye uchumi wa kati.
Changamoto nyingine: Ni pamoja na vijana kutokidhi vigezo vya mikopo vilivyowekwa na taasisi za kifedha, upatikanaji mdogo wa mitaji na fursa za biashara, matumizi ya dawa za kulevya, upungufu wa malezi na mwongozo stahiki, athari za shinikizo rika, matumizi yasiyo sahihi ya mitandao ya kijamii, na kuongezeka kwa tatizo la afya ya akili.
Kwa kutambua changamoto za vijana, Serikali imefanya jitihada mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutunga Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 (Toleo la 2024) na kutekeleza programu mbalimbali za uwezeshaji kwa vijana.
Pamoja na jitihada hizo, changamoto za vijana zimeendelea kuwepo. Kwa kutambua hilo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifanya uamuzi wa makusudi na kuanzisha Wizara maalum kupitia Tangazo la Serikali Na. 685 na 686 linalotoa mgawanyo wa majukumu ya Wizara, ambayo majukumu yake ni:
Kuandaa, kuratibu, na kusimamia utekelezaji wa sera zinazohusu maendeleo ya vijana.
Uratibu wa maendeleo ya vijana na dhana ya kujitolea.
Uratibu wa elimu ya uraia kwa vijana na ustawi wa vijana.
Ushirikishwaji na uwezeshaji wa vijana kiuchumi.
Uratibu wa majukwaa ya vijana.
Kuboresha utendaji wa maendeleo ya rasilimali watu na kusimamia taasisi zilizo chini ya ofisi.
Katika kusimamia programu za uwezeshaji vijana kiuchumi, Wizara imetoa mikopo ya vifaa yenye thamani ya shilingi milioni 824,463,770 kwa vijana 126 katika mikoa ifuatayo:
Mwanza: Vijana 39
Mtwara: Vijana 40
Mbeya: Vijana 22
Rukwa: Vijana 10
Arusha: Vijana 15
Mikopo hii imetolewa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili kuwawezesha vijana kujiajiri na kuajiri wengine.
Aidha, Wizara imeendelea kuboresha mifumo ili kupunguza changamoto na vikwazo vilivyokuwepo hapo awali. Maboresho hayo ni pamoja na:
Utoaji wa Mikopo: Sasa mikopo inatolewa kwa vikundi na pia kwa kijana mmoja mmoja.
Kipindi cha Neema (Grace Period): Mikopo sasa ina kipindi cha neema cha kuanzia miezi mitatu hadi miezi sita.
Sekta za Kipaumbele: Kwa miradi maalum ya kilimo, uvuvi, na ufugaji, kipindi cha neema ni miezi minane.
Riba: Riba imepunguzwa hadi kufikia 5% kwa kipindi chote cha mkopo.
Uwezeshaji wa Vifaa: Wizara imejikita zaidi kwenye uwezeshaji wa vifaa badala ya fedha pekee.
Wizara imeingia makubaliano na taasisi za kifedha kwa ajili ya kutoa mikopo na mafunzo kwa vijana. Wanufaika hupatiwa mafunzo katika hatua tatu muhimu:
Kabla ya kupata mkopo.
Wakati wa kupata mkopo.
Wakati wa mchakato wa uzalishaji.
Katika kutekeleza ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan, aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2025:
Tarehe 5 Februari 2026, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana ilikabidhiwa hundi ya shilingi bilioni 200 kwa ajili ya uwezeshaji wa vijana.
Fedha hizi zinatolewa kupitia sekta mbalimbali kama vile kilimo, madini, mifugo na uvuvi, viwanda na biashara, habari, utamaduni, sanaa na michezo, elimu, sayansi na teknolojia, pamoja na maendeleo ya jamii.
Hadi kufikia Aprili 2026, jumla ya maombi 30,384 ya mikopo ya miradi ya vijana yamepokelewa na yanafanyiwa uchambuzi.
Katika awamu ya kwanza, kiasi cha shilingi bilioni 48.6 kimetolewa, kikitarajia kunufaisha vijana takriban 10,000.
Katika awamu ya pili, kiasi cha shilingi bilioni 2.5 kimepokelewa kwa ajili ya kunufaisha vijana 888 kupitia miradi 36, jambo litakalozalisha ajira 4,440.
Katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana, Wizara imetekeleza programu zifuatazo za ukuzaji ujuzi:
Mafunzo kwa Njia ya Wanagenzi: Mafunzo haya yametolewa kwa vijana 5,746 katika vyuo na taasisi za mafunzo 46 nchini.
Mafunzo ya Uzoefu wa Kazi (Internship): Kupitia njia ya utarajali, vijana 2,500 wamepatiwa mafunzo haya.
Fursa za Ajira Nje ya Nchi: Vijana 7,826 wamepatiwa mafunzo maalum ya kushindania fursa za ajira ndani na nje ya nchi.
Wizara itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha vijana wanapata ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira kwa sasa.
Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana kwa kushirikiana na Wizara ya Vijana, Ajira na Uwezeshaji Zanzibar, imeratibu uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru tarehe 2 Aprili 2026 katika Uwanja wa Gombani, Pemba.
Mgeni rasmi alikuwa Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika mikoa 31 na halmashauri 195 nchini. Kaulimbiu ya mwaka huu ni: "Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja kuleta Maendeleo."
Kupitia mbio hizi, wananchi wanahamasishwa kupambana na dawa za kulevya, malaria, UKIMWI, rushwa, na kuzingatia lishe bora.
Pamoja na mafanikio yaliyopatikana, Wizara inakabiliwa na changamoto zifuatazo:
Ongezeko la mahitaji ya mikopo kulinganisha na kiasi cha fedha kinachotengwa. Upungufu wa ujuzi miongoni mwa vijana unaoendana na soko la ajira. Uelewa mdogo wa stadi za maisha, uzalendo, na masuala ya afya ya uzazi na akili.
Mikakati na Mipango ya Baadaye (2026/2027)
Ili kukabiliana na changamoto hizi, Wizara imejipanga kutekeleza mikakati ifuatayo:
Ushirikishwaji wa wadau: Kuongeza bajeti ya programu za vijana kupitia wadau wa maendeleo. Elimu ya Mikopo: Kutoa elimu zaidi kuhusu masharti na fursa za mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Vituo vya Maendeleo ya Vijana: Kutoa mafunzo ya muda mfupi ya kilimo, ujasiriamali, na TEHAMA.
Mfumo wa Kidijitali wa Vijana: Kuandaa mfumo wa kuratibu masuala ya vijana utakaosaidia kukusanya taarifa, sifa, na ujuzi wa vijana ili kuwaunganisha na fursa za ajira na mikopo kwa urahisi zaidi.
Wizara inaamini kuwa kupitia mifumo hii mipya, vijana wengi zaidi watafikiwa na kuwezeshwa kuinua hali zao za kiuchumi na kijamii.
Kiasi cha Tsh. 30,104,264,000 kimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ambapo:

Makadirio ya Bajeti ya Maendeleo ya Vijana (2026/2027)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana inaomba kuidhinishiwa jumla ya Tsh. 35,957,298,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo kama ifuatavyo:Kiasi cha Tsh. 30,104,264,000 kimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ambapo:
- Mishahara: Tsh. 1,227,961,000.
- Matumizi Mengineyo (OC): Tsh. Bilioni 28,876,303,000.
- Fedha za Ndani: Tsh. 5,000,000,000
- Fedha za Nje: Tsh. 853,034,000