Wizara ya Viwanda na Biashara, taarifa zao za bei za mazao siyo sahihi.

Wizara ya Viwanda na Biashara, taarifa zao za bei za mazao siyo sahihi.

Shebbydo

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
1,174
Reaction score
1,937
Habari Wana JF,

Katika website ya wizara ya viwanda na bishara, kuna kipengele ambacho huwa wanaweka taarifa za bei za mazao hasa ya vyakula. Hii huwa ni madhumuni ya kumsaidia mfanyabiashara kujua bei katika mikoa mbalimbali zipoje. Lakini katika utafiti wangu nimegundua taarifa hizi hazina ukweli, mfanyabiashara ukizifuata utaumia.

Nimefikia kulijua hili ni baada ya kufuatilia bei ya ngano Mwanza. Katika taarifa yao ya tar 5 Dec 2016, wanasema bei ya jumla ya ngano kwa kilo mia ni shilingi za Kitanzania laki moja na sabini(170,000). Jambo hili si kweli. Bei ya ngano kwa jumla, kwa mfuko wa kilo 25 ni Tsh 28,000 hadi 30,000. Kwa maana hiyo kilo mia ni Tsh 120,000, hiyo 170,000 imetoka wapi? Haya kwa bei ya rejareja ngano kilo moja ni Tsh 1,400, kilo mia kwa bei ya rejareja itakuwa ni Tsh 140,000 bado hiyo 170,000 haifiki. Hilo soko wao wamelitoa wapi? Huo ni upotoshaji, hasa wa taarifa muhimu ambazo mfanyabiashara anazihitaji.

Rai yangu kwao hawa wahusika, kama kweli wanataka kutoa taarifa za kuwasaidia Watanzania, watafute habari zenye ukweli ili watoe bei zilizopo sokoni na si kukaa ofisini na kutunga bei za kufikirika.
 
Sijasoma hizo bei za wizara ila na wewe hapa umetuletea kipande tu cha hadithi kama ambavyo LABDA na wizara imefanya. Bei ili ieleweke lazima iseme MUDA au kipindi iliyopigiwa hesabu, MAHALA ambapo bei hiyo inahusika, na MKOKOTOO uliohusika.

Mambo hayo matatu yanaweza yakahalalisha bei ya wizara na papo hapo kuhalisha bei uliyoiona wewe. Kumbuka hakuna bidhaa duniani yenye bei moja.
 
Itakuwa nimesahau kuandika ni taarifa ya lini. Hii ni taarifa ya tar 5 Dec 2016
 
Hizo bei za wizara ni wastani au? Kama wizara wametoa bei ya wastani upo uwezekano kwamba wako sahihi na kwamba upo pia uwezekano kwamba na wewe bei zako ziko sahihi kwasabu wastani unatabia mbaya ya kuzibwaga bei zilizo chini yake na bei zilizojuu yake.
 
Ni vigumu kujua kama ni za wastani ama vipi kwa sababu title yake inasema "WHOLESALE PRICES FOR FOOD CROPS IN Tsh/100kg". Lakini pia nimejaribu kuuliza katika wilaya zingine za mkoa Mwanza sijapata wastani ambao unaweza kuleta bei yao.
 
Okay, mkuu hapo tena siwezi kuwa wa msaada! Nitabaki kushangaa kama wewe.
 
Hawa inabidi wakapumzishwe tu maana kazi hawawezi......vijana kibao wapo mtaani wanahitaji kufanya kazi kwa bidii na umakini. Sasa ya nini kukumbatia wazee wa mwaka 47 kufanya kazi za vijana
 
Back
Top Bottom