Wizara yawafunda wananchi kutambua Asali `feki`

Wizara yawafunda wananchi kutambua Asali `feki`

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
wizara(1).jpg

Wizara ya Maliasili na Utalii


Wizara ya Maliasili na Utalii imewafunza wananchi

namna ya kubaini Asali isiyokuwa halisi ambayo

inadaiwa kutengezwa na wafanyabishara kwa

kutumia maji ya miwa yaliyochemshwa na

kubadilika kuwa sukari guru.

Akizungumza NIPASHE katika maonyesho ya

biashara ya 37 yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar e

Salaam jana, Ofisa nyuki na wakala wa huduma za misitu kutoka wizara hiyo,

Theresia Kamote, alisema kuna njia kadhaa za kuitambua asali iliyochakachuliwa.

Kamote alizitaja njia hizo kuwa ni pamoja na kuweka maji kwenye glasi na kisha

kumimina Asali na kwamba ikikaa chini ya glasi bila kuchanganyana na maji basi hiyo ni asilia na inakuwa haijachanganywa na chochote.

Alisema njia ya pili ni kuiweka Asali kwenye njiti ya kibiriti na kisha kuiwasha ikiwa

njiti hiyo itawaka basi Asali haijachakachuliwa kwa kuchanganywa na chochote lakini njiti ya kiberiti isipowaka inakuwa ni feki.

Aidha, Kamote aliongeza kuwa wizara yake imekuwa ikiwasisitiza wafanyabiashara

wa bidhaa hiyo kuwa waaminifu na kuwauzia wateja waoe bidhaa halisi na wale ambao bidhaa zao zinagundulika zimechakachuliwa ziharibiwa.

Aliongeza kuwa njia nyingine ni kuonja bidhaa hiyo na kwamba iliyokachuliwa kwa

kuchemsha inatoa harufu ya moshi tofauti na ambayo ni halisi.

"Wizara imekuwa ikitoa rai kwa wafanyabiashara wa bidhaa hiyo kuwa waaminifu na

pale tunapogundua bidhaa yenyewe ni feki sisi kama wizara huwa tunaiharibu,"

alisisitiza Kamote.




CHANZO: NIPASHE

 
kabanga hii njia ninaifahamu miaka mingi iliyopita
hii husaidia kujua asali iliyoongezwa vimiminika kama maji au sukari guru
lakini kwa asali yenye sumu au kitu ambacho siyo cha kawaida siyo rahisi kuitambua kwa kutumia hiyo njia.
hii itasaidia sana watu wasiziwe asali iliyoharibiwa....
 
Last edited by a moderator:
kabanga hii njia ninaifahamu miaka mingi iliyopita
hii husaidia kujua asali iliyoongezwa vimiminika kama maji au sukari guru
lakini kwa asali yenye sumu au kitu ambacho siyo cha kawaida siyo rahisi kuitambua kwa kutumia hiyo njia.

kwakweli sikuwa na fahamu, nilikuwa nikihitajia asali naagiza kutoka shamba kabisa...
 
.. Asante sana kwa kutufumbua macho! Leo nilimuuliza jamaa ya kuhusu hili jambo! Akanieleza kuwa ni vigumu kutambua feki na asili.
...JF bigup !
 
Back
Top Bottom