Wizi katika Biashara za Mtandoni

Wizi katika Biashara za Mtandoni

Whk

Member
Joined
Oct 1, 2020
Posts
77
Reaction score
76
Biashara Za Mtandaoni zinatusaidia sana kupata vitu kwa bei rahisi sana Ila sasa Biashara hii imeingiliwa na Matapeli wengi. Sasa utamjuaje uyu ni tapeli.?

JINSI YA KUMJUA TAPELI WA MTANDAONI

1. Mabadiliko ya namba za simu za huduma kwa mteja.
Yaani kila ukiperuzi bidhaa utakuta baada ya muda fulani utakuta namba mpya.

2. Kwa mtandao wa Instagram kunakuwa na limit ya kucomment kwa maana huwezi kucomment bidhaa inayotangazwa

3. Kwenye Mtandaoni instagram huwezi kuona mtu anatangaza duka hilo,kwa mfano "karibu hapa duka fulani tunauza bidhaa fulani.

4. Hutakuta Lipa namba Matapeli wengi wanataka uwatumie kwenye namba zao za simu.

5 .Utakuta bidhaa imepigwa picha ila quality ya picha ni ndogo hii ni kwasababu wanadownload izo picha kwenye profile za instagram au facebook za watu wengine.

HiVYO VITU NIMEVIONA KWA MTU FULANI BAADA YA KUTAPELIWA

Ushauri Kwa serikali kama wameweza kuzuia picha za ngono x zisionekane Mtandaoni basi wazuie ili jambo kwa kwa kila mtu anayetaka kuweka bidhaa yake mtandaoni basi shariti ilo tangazo lipewe kibari TCRA.

Lengo Line za simu zisajiliwe kwa kutumia namba ya NIDA litimie.
 
Lengo Line za simu zisajiliwe kwa kutumia namba ya NIDA litimie.
Hii hoja baso inahitaji ufafanuzi.
1. Mabadiliko ya namba za simu za huduma kwa mteja.
Yaani kila ukiperuzi bidhaa utakuta baada ya muda fulani utakuta namba mpya.

2. Kwa mtandao wa Instagram kunakuwa na limit ya kucomment kwa maana huwezi kucomment bidhaa inayotangazwa

3. Kwenye Mtandaoni instagram huwezi kuona mtu anatangaza duka hilo,kwa mfano "karibu hapa duka fulani tunauza bidhaa fulani.

4. Hutakuta Lipa namba Matapeli wengi wanataka uwatumie kwenye namba zao za simu.

5 .Utakuta bidhaa imepigwa picha ila quality ya picha ni ndogo hii ni kwasababu wanadownload izo picha kwenye profile za instagram au facebook za watu wengine.
#6. Elimu kwa uma itolewe mara kwa mara, Uma ukiwa na ufahamu wa kutosha mataperi watapungua.

// AI spoiler | Bofya hapo chini kwa Vidokezo vya kujilinda.
Kumjua tapeli wa mtandaoni ni muhimu sana ili kuepuka hasara na usumbufu. Hapa kuna viashiria vinavyoweza kusaidia kutambua matapeli wa mtandaoni:

1. Kubadilisha namba za mawasiliano mara kwa mara: Matapeli wengi hawatumii namba thabiti kwa huduma zao, badala yake hubadilisha namba mara kwa mara, ili wasitambulike au kufuatiliwa.

2. Maoni au maingiliano yaliyodhibitiwa kwenye Instagram: Akaunti za ulaghai mara nyingi huzuia watu kuacha maoni kwenye bidhaa zao au matangazo, ili wasiulizwe maswali au wasifichuliwe.

3. Kutokuwa na anwani au maelezo ya wazi ya duka: Matapeli mara nyingi hawana taarifa kamili kuhusu biashara zao, kama vile mahali duka linapopatikana au maelezo ya kina ya bidhaa.

4. Kutumia namba za simu binafsi badala ya namba rasmi za malipo: Badala ya kutumia huduma salama kama "Lipa namba," wanakuhimiza utume pesa moja kwa moja kwenye namba zao binafsi.

5. Ubora duni wa picha za bidhaa: Picha wanazotumia mara nyingi huchukuliwa kutoka kwa akaunti nyingine za mitandao ya kijamii, na zina ubora wa chini au hazionyeshi bidhaa kwa uwazi.

6. Madai ya "ushindi" au ofa isiyoeleweka: Wanaweza kudai umeshinda kitu fulani ambacho hujawahi kushiriki, au kutoa ofa ambazo ni nzuri mno kiasi cha kutiliwa shaka.

7. Kuhimiza haraka haraka kufanya malipo: Wanaweza kukuhimiza uharakishe malipo kabla haujachukua muda wa kuthibitisha uhalali wa biashara.

### Vidokezo vya kujilinda:
  • Hakikisha uhalali wa biashara: Tafuta maoni ya wateja wengine na uhakiki taarifa za biashara kwa kina kabla ya kununua bidhaa.
  • Tumia malipo salama: Hakikisha unatumia njia zinazoweza kufuatiliwa kama "Lipa namba" au miamala rasmi ya benki.
  • Usitoe taarifa za siri: Kamwe usitoe nywila au taarifa nyeti kwa mtu yeyote usiyemjua.
  • Ripoti vitendo vya utapeli: Tuma neno "Utapeli" kwenda namba 15040 ikiwa unashuku unatapeliwa.

Kwa maelezo zaidi au msaada, unaweza pia kufuatilia kampeni za TCRA na Jeshi la Polisi zinazolenga kuongeza elimu kuhusu uhalifu wa mtandaoni.
 
Mkuu umeeleza FACTS, lakini changamoto kubwa sana iliyopo ni elimu ya biashara ya mtandao.
Ni rahisi sana kwa watu walio nje ya mkoa wa Dar kutapeliwa kwasababu ya misingj, maadili na malezi waliokulia huko mikoani mfano Nyanda za juu kusini, kaskazinj na kanda ya ziwa
Hizo sehem mtu huamini “word of mouth” bila kuuliza mara mbili mbili maana huko hakuna janjajanja kama za vijana wa Daslaam

Inahitajika elimu ya “e commerce” ili kuweza kufahamu hapa napigwa au la,

Kusajiki namba kwa NIDA tu bado haijaokoa tatizo la namba feki
Nashauri kama raia wa Tanzania aruhusiwe kutumia LINE ya simu MOJA ambayo imesajiliwa na NIDA na kua na taarifa zinazolink na RITA, TRA, SERIKALI ZA MITAA TPF ELIMU YA JUU na IMMIGRATION hizi taarifa ziwe current na iwe lazima mtu kuUpdate address ya makazi kila baada ya miezi mitatu.
Kwa kuongezea hii Namba ya simu ndio itumike kama utambulisho kwasababu itakua imebeba taarifa zako zote “current”
 
Back
Top Bottom