Wizi kwenye account ya mteja bank.

samike

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2012
Posts
609
Reaction score
236
Wakuu naombeni msaada wenu, Kuna mteja wa Bank moja wapo hapa tanzania yeye amefika bank akabaini kuwa salio lake limepungua kupita kiasi, baada ya kufuatilia akajibiwa kuwa fedha yake imetolewa Dar es salaam ndani kwa Teller kiasi cha Tsh. 3,000,000/= wakati yeye hata Dar es salaam hajawahi kufika na kadi anayo nyumbani kwake Tabora maelezo ya awali ya meneja Tawi anasema hilo ni tatizo la kwao na walimwahidi kumrejeshea fedha hizo lakini sasa huu ni mwezi umepita na hela yake haijarudishwa, wakuu tunaombeni msaada wa kisheria, mteja huyu afanyaje nini, haki zake zipi.Nawasilisha.
 
Asiishie kuongea na benki kwa simu, aweke madai yake kwa maandishi. Benki zetu zinapishana kiutendaji, wengine mpaka wapitishiane majalada na approval zao, ni zaidi ya mwezi.
 
Rafiki yangu
Mie niliibiwa fedha zangu bank mwezi wa pili 2013, kutoka kwenye bank zinazoo jiita za kimataifa..teh teh..wakachunguza wakaniambia hela ziliibiwa kutokea uingereza, wakahitaji passport yangu na document nyingine huwezi amini ni miezi sana sasa imepita na sijarudishiwa fedha zangu.
Kila siku njoo kesho njoo kesho mpaka nimechoka..
nitatafuta ushauri wa kisheria halafu nitakujulisha kwani mie nataka nitumie media kuwatangaza na kuhakikisha endapo kesi ikisomwa kila siku iwe hiyo benk inaandikwa kwenye magazeti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…