Wakuu naombeni msaada wenu, Kuna mteja wa Bank moja wapo hapa tanzania yeye amefika bank akabaini kuwa salio lake limepungua kupita kiasi, baada ya kufuatilia akajibiwa kuwa fedha yake imetolewa Dar es salaam ndani kwa Teller kiasi cha Tsh. 3,000,000/= wakati yeye hata Dar es salaam hajawahi kufika na kadi anayo nyumbani kwake Tabora maelezo ya awali ya meneja Tawi anasema hilo ni tatizo la kwao na walimwahidi kumrejeshea fedha hizo lakini sasa huu ni mwezi umepita na hela yake haijarudishwa, wakuu tunaombeni msaada wa kisheria, mteja huyu afanyaje nini, haki zake zipi.Nawasilisha.